22.11.13

Friday, August 06, 2010

THE MAKING OF FUNGENI MIKANDA "CHEGE & Mh TEMBA"

Muda mfupi uliopita usiku huu nilikuwa kwenye utengenezaji wa video mpya ya Chege na Temba pale maeneo ya Sinza Mori stand ambapo kwa sasa kuna kituo kipya cha kuweka mafuta kinaitwa BIG BON kina mda wa siku 4 toka pamefunguliwa.

Wimbo huo ukijulikana kwa jina la FUNGENI MIKANDA video yake ilikuwa ikishutiwa na Visul lab NEXT LEVEL chini ya mtu mzima Adamu Juma.

Baada ya ubishi wa mda mrefu atimae nilimfuma mtu mzima KR akipigwa mapodaaaaaa ili atoke freshiii.

Pembeni kushoto ni Producer DUNGA, TEMBA na CHEGE wakishikana mkono kuashiria kumaliza salama kwa video hii sasa kilichobaki ni kusikiliza uliaji wake kama wimbo wa taifa

Nilimuuliza Chege kwanini mnatoa nyimbo kwa mfululizo na kila mkitoa wimbo inapanda chat za juu..akanijibu
HUU NI MUDA WA HELA HAKUNA KULAZA DAMU WAKATI MWILI UMECHANGAMKA.

No comments: