22.11.13

Thursday, September 09, 2010

MRISHO MPOTO AJA NA ADELA

Msanii mwenye mistari yenye ujumbe mzuri na kumfikia mtu kwa haraka ujumbe wake Mrisho Mpoto, ametoa wimbo wake mpya kama wiki na nusu sasa unaoitwa Adela akiwa amemshirikisha msanii Ismail aliyeimba kiitikio cha wimbo huu.
Wimbo huu Mpoto anamzungumzia Adela kwamba anyooshe kidole na hana nia mbaya yakumrudisha darasani, Studio ya Fishcrab chini ya Producer Lamar ndio umeutengeneza wimbo huu.
Ufuatilie wimbo huu mpya wa Mpoto ili upate na wewe ujumbe uliopo ndani ya wimbo huu wa Adela.

7 comments:

Anonymous said...

Mrisho umetishaaaaa

G said...

kaka nakukubali sana...wewe ndio utastahili kuuitwa msanii...ujumbe umefika kwa walengwa

Anonymous said...

safiiii.....

Anonymous said...

uko level ya kimataifa sana kaka...

Anonymous said...

jamani kwani wimbo huu unapatikana kwenye album ile ya kwanza au mpya

Anonymous said...

jamaa anaweza mbaya,kama vipi mpoto wauzie mashairi wauza sura............

Anonymous said...

thats it wow nice