22.11.13

Tuesday, October 18, 2011

FILAMU KUBWA YA CPU KUZINDULIWA RASMI 24/11/2011 KATIKA SINEMA.

 
Dar es  salaam, October 18, 2011
Imetayarishwa na Haakneel Production
wakishirikiana Wegos Works,
ikiogozwa na Karabani,
kuandikwa na Novatus Mugurusi.
Mratibu wa  Filamu ya CPU, Bw Evans Bukuku amesema kuwa  Filamu hiyo inalenga kuburudisha na kuelemisha jamii kwa ujumla. ikiwa imechezwa hapa hapa Dar es salaam katika maeneo tofauti ya jiji, ili  kuleta uhalisia zaidi.  Filamu ya CPU ni mwanzo wa mapinduzi makubwa ya kihistoria katika tasnia ya filamu hapa Tanzania na Afrika. Ikiwa imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu katika Picha, sauti, uigizaji kiujumla kila kilichofanyika ndani ya CPU kimefanywa kwa umakini na utashi wa aina yake. Mpaka sasa tunaweza kusema CPU ni miongoni mwa Filamu chache sana zilizoweza kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu hapa Afrika.
CPU Ni aina ya filamu ya kipelelezi yaani “Investigatory story” ikiwa  inazungumzia kitengo kilichoundwa kwa ajili ya kufuatilia na kutatua matatizo mbali mbali wakati jukumu lao la kwanza ni kufuatilia juu ya mtoto mchanga  aliyeokotwa pasipo kufahamika ni wa nani. Hivyo Maria Isabela (Sauda Simba) anateuliwa na serikali kuongoza timu  hiyo,  katika hilo inabidi awashawishi watakao msaidia ambao ni Alex Kibera(Nkwabi Juma) jambazi suguanayetumikia kifungo cha miaka 30 jela, David Kifati(steven Sandhu) mtaalamu wa kompyuta na kijana mwenye uelewa mkubwa ambaye anatoka katika familia bora na anayependa anasa.
Pia kuna Rehema Mlaki (Subira Wahure) akiigiza kama msichana anyefanya kazi ya uwakili wa kujitegemea. Wanaanza kazi ya kwanza ambayo kiujumla ni yenye misukosuko na inayohitaji umakini wa hali ya juu kwa kuwa ni ya hatari sana  hasa wanapokabiliana na mtu kama Jibaba(Mobby Mpambala) mmiliki wa danguro kubwa hapa jijini na mzoefu wa biashara haramu. Pia kuna mambo mengine mengi ya ajabu  wasiyotarajia Kiujumla ni Filamu yenye mjumuisho wa matukio mengi ya kusisimua na kufurahisha.
Filamu kubwa ya CPU imeandikwa na mwandishi mahiri wa Script Novatus Nago Mgurusi na kuongozwa na muongozaji wa filamu wa Kimataifa Karabani, ndio filamu ya kwanza yenye ubora wa kuonyeshwa katika majumba ya sinema Ulimwenguni.
Katika Filamu hii kuna waigizaji wengine mahiri wengi ambao ni waigizaji wakuu wasaidizi wapatao 30 humu kuna watu kama Dotnata (Husna Posh), Jengua (Mohamed Fungafunga) , hashim Kambi, Dude (kulwa kikumba), Richard Masinde na wengine wengi. Pia kuna waigizaji wa nyongeza (Extras) wapatao 300, tunaamini hii ni filamu ya aina yake kwa yeyote yule atakayeitazama hakika atathibitisha hili.
CPU itazinduliwa katika sinema pale New World Cinema Mwenge tarehe 24 Novemba 2011 saa moja kamili jioni na kuoneshwa kwa wiki nzima kuanzia tarehe 25 Novemba 2011 pale Mlimani city cinema century kila saa moja jioni.Baada ya hapo CPU itaoneshwa Bure katika maeneo ya wazi Dar es Salaam,  Mbeya, Arusha, Mwanza,  Zanzibar na Dodoma. Pia itapatika katika DVD.
Unaweza kuanza kufanya booking ya Ticket yako kuanzia sasa kupitia namba 0715 CINEMA / 0753 CINEMA (CINEMA = 246362)
Kwa taarifa zaidi juu ya filamu ya CPU na uzinduzi wake utapata kupitia vyombo mbali mbali vya habari pia unaweza kufuatilia zaidi kupitia tovuti ya www.cpu.co.tz au www.filamucentral.co.tz
Asanteni
Sauda Simba muusika mkuu katika Filama ya CPU

2 comments:

Anonymous said...

Tanzania Film Critics Association tunawapongeza sana kwa juhudi ambazo zimeonyeshwa katika kuitengeneza hii Filamu,tunaamini kabisa kuwa mageuzi haya yataleta changamoto ya msingi na yata thaminisha kazi za Filamu katika thamani halisi,Ni changamoto kubwa kuanzia kwa wasanii wenyewe,wasimamizi wa kurekodi hadi wasambazaji wa kazi za Filamu kuhakikisha ubora ambao utahakikisha mwisho wa siku kipato kizuri kitokanacho na Filamu husika.Sisi tunaamini kuwa Filamu nzuri ni ile yenye usimamizi mzuri unaotokana na wazo zuri ,hadithi nzuri na utayarishaji mzuri.Hongera kwa wote walioshiriki katika Filamu hii,Wasalam Emmanuel N.M.Manase

Anonymous said...

I just saw the teaser, it is awsome. Please upload more trailers. Can't wait, I think I might just have to fly down to Dar from ATL just to be there for the showing!!! Good Job TZ