22.11.13

Wednesday, October 26, 2011

KIPINDI KIPYA CHA RUNINGA (MSETO EAST AFRICA)

Mtangazaji maarufu toka nchini Kenya,Mzazi Willy M. Tuva anayefanya kipindi cha miziki ya kizazi kipya katika Radio Citizen ameanzisha kipindi cha runinga kinachoiunganisha AFRICA MASHARIKI kimziki.Kipindi hicho kwa jina MSETO EAST AFRICA kinakwenda hewani kila Jumatatu hadi Ijumaa (4.15 – 5 Jioni) katika CITIZEN TELEVISION
Kipindi cha MSETO EAST AFRICA kinacheza video za wasanii toka Kenya,Tanzania,Uganda,Rwanda,Burundi na Sudan kusini katika runinga inayozidi kusambaa katika mataifa yote ya Afrika Mashariki na kati. Kipindi hiki Kinaongozwa na MZAZI WILLY M TUVA na DJ FLASH pia kinawapatia wasanii Chipukizi nafasi. Wadau mnaombwa kushirikiana kufanikisha umoja wa Afrika Mashariki kupitia mziki. Wasanii wa TANZANIA wanaweza kutumia kipindi hiki KUJITANGAZA Kenya na AFRIKA MASHARIKI. Wasiliana na mzazi kwa email: msetoeastafrica@gmail.com au jiunge na facebook fan page ya MSETO EAST AFRICA 

No comments: