22.11.13

Wednesday, January 11, 2012

REST IN PEACE MZEE KIPARA

Mwigizaji wa siku nyingi Tanzania, Mzee kipara amefariki leo kwenye nyumba ya KAOLE SANAA GROUP ambapo alikua anaishi, kutokana na maradhi mbalimbali pamoja na utu uzima ambapo alianza kuugua zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
 
Mzee Kipara alikua miongoni mwa waanzilishi sita wa KAOLE SANAA GROUP mwaka 1999, ambapo wengine ni Marehemu RAJABU HATIA (MZEE PWAGU), MAMA HAMBILIKI, Bi HINDU, ZENA DILI, CHRISANT MHENGA ambapo mchezo wa kwanza wa kikundi hicho kuoneshwa ITV, uliitwa HUJAFA HUJAUMBIKA ambapo Mzee kipara alikua anacheza kama Baba mzazi wa DR CHENI wakati huo Dr CHENI anataka kumuoa KISSA ambae alikua binti mlemavu.
 
kabla ya kifo chake, mwigizaji huyo alishazushiwa kifo zaidi ya mara moja, ambapo mara ya mwisho ilikua ni NOVEMBER 10 mwaka jana.
 
Mwili wa Mzee KIPARA utazikwa kesho Kigogo Dar es salaam , kwa mujibu wa mwenyekiti mstaafu wa KAOLE Sanaa Group CHIKI.

No comments: