22.11.13

Sunday, February 19, 2012

Airtel Mgagao network launch

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Bi Thresia Msuya akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya
Airtel katika wilaya ya Mwanga kijiji cha Mgagao ambapo mnara huo
utatoa huduma ya mawasiliano kwa zaidi ya vijiji vinne wilayani hapo.
Toka kushoto wakwanza ni Afisa mauzo wa Airtel Mwanga Semshitu Msangi
na nyuma ni Diwani wa kijiji hicho Bw Mohamed Gendiwa pamoja na
viongozi wengine wa kijiji cha mgagao mwishoni mwa wiki

PRESS RELEASE
Airtel yazindua huduma za Mawasiliano Mgagao wilayani Mwanga
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania imezindua huduma za
mwasiliano ya simu za mkononi katika kijiji cha mgagau wilayani Mwanga
mkoani Kilimanjaro ambapo mawasiliano hayo yatafikia vijiji 4  vya
jirani  vikiwemo Makungwini, Mambarale, Kingondi, na pangalo
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mawasiliano hayo, Afisa  Mauzo kanda
ya kaskazini Semshitu Msangi alisema ”Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel inaendelea kuwajali na kuwahakikishia watanzania walio sehemu
mbali mbali za  vijijini na mijini mawasiliano bora na kwa bei nafuu .
Airtel tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kuboresha ulinzi,
kukuza uchumi, kuweka jamii pamoja na kwa kutambua hilo, tumewekeza
zaidi katika kupanua huduma zetu za mawasiliano hasa vijijini ambapo
ndiko kwenye changamoto kubwa”
Sasa wakazi wa  kata ya Mgagao na vijiji vya jirani wanaweza kupata
huduma zetu zote zinazopatikana nchi zima kwa kuhamia Airtel sasa,
huduma hizi ni  kama vile za pesa mkononi kutuma na kupokea fedha
“Airtel Money” , huduma za internet, pia kupata viwango vya kupiga na
kutuma sms vya bei nafuu na kupata huduma bora na ya haraka ya
internet zilizoenea zaidi nchini zima, Aliongeza Msangi.
Kwa niaba ya wananchi wa  kijiji cha mgagao mweneyekiti wa Halmashauri
ya Mwanga Theresia Msuya alisema ”nashukuru Kampuni ya simu ya Airtel
kwa kutufikishia mawasiliano wilayani Mwanga na kushiriki katika
kutatua changamoto za mawasiliano tuliizokuwa tunazipata, pia
kutuondolea adha  ya kutokuwa na mwasiliano ya uhakika pale tunapotaka
kuwasiliana. Nachukua fulsa hii kuwaasa wananchi wa mgagau kutumia
fulsa hii ya pekee ambayo wameipata toka Airtel katika  kufanikisha
shuguli zao za biashara na za kiuchumi ili kukuza  maendeleo ya wilaya
ya mwanga”.
Uzinduzi wa mawasiliano ya mgagau yatawezesha pia vijiji vya jirani
vya  Makungwini, Mambarale, Kingondi, na pangalo pia kufikiwa na
mawasiliano .tuna shukuru  Kampuni ya simu ya Airtel kwa kutuletea
mwasiliano ya uhakika yenye wigo mpana na hivyo kuwa na uhakika wa
kuwasiliana  popote pale uendapo Airtel iko na wewe. Aliongeza
Theresia.
Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mawasiliano
ya simu za mkononi yanawafikia watanzania wote nchini nzima hasa walio
vijijini
End

No comments: