22.11.13

Friday, February 03, 2012

KATI YA TIMBULO NA KUNDI LA X MALEYA NANI KAMGELEZEA MWENZAKE????

Msanii kutoka bongo anayejulikana kwa jina la Timbulo ambaye alitoka na wimbo wake wa kwanza unaojulikana kwa jina la Domo Langu na wa pili Waleo wa Kesho na kuteka wabongo wengi sana, sasa imegundulika kuwa jamaa amewacopy wasanii X  Maleya kutoka Cameroon. Bado sijajua je mwenye makosa ni producer wake aliyemtengenezea biti anajulikana kama Lil Gheto au ni yeye Timbulo ndio aliyempa melody producer?
Mimi nataka msikilize jinsi nyimbo zilivyofanana halafu uniambie ukiwa kama mdau unayependa mziki wa bongo fleva ufikke mbali kimataifa zaidi.

Hawa ndio wasanii wanaojulikana kwa jina la X MALEYA kutoka Cameroon 

TIMBULO ALIANZA KUTOKA NA HII:

HALAFU SIKILIZA HII ILIYOTOKA 2009

Halafu haitoshi ndugu yetu akaja akatoa wimbo huu tena

HALAFU SIKILIZA NA HII

19 comments:

Anonymous said...

Choka hapa kila kitu kinafanana na Kama hajawacopy washkaji why nyimbo zake zote mbili zifanane na washkaji?ni uvivu tu wa kufikilia walionao wasanii wetu wa bongo ndomana hawadumu ktk game.Wao wanachofikilia watoe nyimbo ili wapate mademu na si kua na maisha mazuri.

Anonymous said...

yaani choka,hapo moja kwa moja timbulo ndie mwiz wa kazi za watu haiwezekan nyimbo zote yy akopy na kupaste 2,pia huyo prodyusa wake nae ni mjinga inabidi achekeche akili sio ategemee wenzie watoe then yy ndio achukue,bora ingekuwa ni beat 2 hadi sauti na madhari yale yale,wabongo tumezidi jaman kama m2 unajijua huwez kimba mpaka uige vya wenzako si lazima wote tuimbe wengine tubaki kuwa mashabiki 2,ni mtazamo wangu 2.

Anonymous said...

Choka hebu tuletee hapa huyo Timbulo na huyo producer wake wajibu mashtaka maana hii aibu kwetu waTz cjui itaisha lini? Hivi hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kumfungia huyu producer, Timbulo na hizo nyimbo zisiruke hewani ili iwe fundisho??? Choka hebu tusaidie hili maana wamezidi hawa

Benmoo! said...

huyo dogo msanii wa bongo nahisi sio msanii but analazimisha mya kulingana na hali ngumu ya maisha, this is stupid, kwa staili hii hatuwezi endelea katika muziki wa bongo. But may be washikaji wa cameroon wamempa shavu arudie nyimbo zao.

Anonymous said...

jamani hata kama Timbulo amecopy si mnaburudika???

hamjui kucopy na kupaste nako ni shughuli??

Anonymous said...

kaka choka hii haina ubishi,kuanzia yeye hadi producer wake wote wezi yaani machizi hawajaacha hata chembe wamekomba vyote du noma

Anonymous said...

KAKOPI,Hapo ngo ukisikia waimbaji wengine ni kama wazamiaji wasojua kuogelea .kakopi hata mtoto mdogo akisikiliza hatotofautisha .Ni sawa na yule alokopi mbagala . huyo atatengeneza mziki kwa mgongo wa wenzake ,Hovyoooo.

Nathan Mhaye said...

Fuck! Jamaa kacopy kila kitu and anajiita msanii na kutolea video basi hata angesema kwamba huwa anacopy kakaa kimya ili apewe sifa kumbe hamna kitu , timbulo sijui producer wote wanatia aibu.. West Africa wanatuzidi kila kitu sasa

Anonymous said...

Mbona JOH MAKINI AMEKU COPY BEAT ZA NYIMBO KIBAO TU,
KILIMANJARO NA BYE BYE HIZI NYIMBO ZA JOH MAKINI AMBAZO AMECOPY TUTOKA KWA WASANII WA WAMEREKANI.
KILIMANJARO - NI BEAT YA SLUM VILLAGE- NYIMBO REUNION
BYE BYE -NI BEAT YA JAY-Z -NYIMBO BROOKLYN WE GO HARDER
SASA HAPA TUMLAUMU NANI AU FAKE /LAZY PRODUCERS AU WASANII,

NikoLiV3 -PHILLY,PA

Anonymous said...

siriiii imefichukaaaaaa!choka eeh hbu tuitie hao wadau wajieleze kwa ufasaha..kukopy gan hukooooo!aibu jmn.

Anonymous said...

Wasanii wa bongo ndivyo walivyo kuanzia hao wa Bongo flava mpaka wa filamu wote ni watu wa kucopy na kupaste halafu wenyewe eti wanadai hati miliki, hati miliki mtaipata wapi wakati wenyewe ndio wezi nambari one?. waangalie vile pumba%*": kabisa. tena huyo dogo hajaacha kitu kabisaaaa mpaka kucheza amecopy na kupaste.

Anonymous said...

Brother choka, kama umeamua kweli kufanya hii kazi ya kuushape mziki i salute you. Ndugu yangu since umeamua kufanya kazi ya ukweli, sasa ni wakati na wewe kuwa muwazi kwa kila kazi utakayo kutana nayo kama hii. Haitakua fare umemuweka msanii kama huyu na wakati kuna wengine kibao pia wanafanya upumbavu kama huu. Nyimbo ya Iveta mfano inatwa nanaa kama sijakosea hiyo beat ni wameiga ya Jeniffer lopez- I'm into you.
Unajua kusema ukweli daima utaonekana adui ila ndo silaha pekee ya kukuweka tofauti na snitch.
Tanzania hamna wanamuziki mpaka producers. na hili lote ni kwa ajili watu hawana knowldge na kile wanachokifanya. ukisikiliza beat za dre ama ma producer wengine you can tell that hii kazi ni ya mtu anaejua anachofanya.
Huwezi pata kazi nzuri toka kwa producer alieacha shule form two, na baada ya hapo akajifunza kiujaujanja fruit loops then anajiita producer.
Mr choka wewe ukiwa kama mtu wa media, ndo kutumia nafasi yako kupunguza huu ujinga na aibu kwa nchi yetu

Anonymous said...

kukopi kdg sio mbaya,sasa jamaa kakopi hadi video locations? Ila jamaa ka hustle mpk cameroon,mpeni haki yake!

Anonymous said...

Kaka tunaomba utuwekee na link za kudownload audio zake hizo original na duplicated za huyo timbulo plz and plz

Anonymous said...

Dogo timbulo ni copy and paste

Anonymous said...

oooops

Anonymous said...

Tatizo wasanii wetu hawajui kuwa technology imekua,watu wanasikiliza nyimbo pia sa sehem nyingine haya kama mambo ya T.i.d nyota yangu,
Angalau kama angesema nimechukua melody na beats kutoka kwa hao jamaa mi nimeweka maneno yangu tu angalau tusingemuona mjinga kaka hivi

Anonymous said...

Kazi ni kazi tu bwana ACHENI KUWAFUATILIA WASANII....ANGALIENI UJUMBE WA NYIMBO....NA SI BEAT ZAKE...WATU WANAJITAHIDI KUTOKANA NA UWEZO WAO....

Anonymous said...

Kwani nyie kimewakera nini? Mbona hata majuu wanacopy? au akikopi timbulo kakosea? acheni hizo bwana