22.11.13

Monday, February 20, 2012

Makamu wa raisi wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano asifu vyombo vya habari TZ

Kulia ni  Nasa Kingu Mkuu wa Vpindi wa East Afrika TV/ Radio
akiwapokea na kutoa maelezo jinsi wanavyofanya shughuli za habari
katika ofisi za East afrika TV/Radio 

Bw Wens Mushi ambae ni Kaiumu Naibu Mhariri wa The Guardian akitoa
maelekezo kwa Makamu wa raisi wa Airtel Afrika kitengo cha mawasiliano
(alieshikilia gazeti) huku Bw Alexander Doll Mkurugenzi mkuu wa
Hill+Knowlton Strategies  (wapili toka shoto) toka  kampuni maalum ya
Mahusiano ya Airtel Afrika akifuatilia kwa undani zaidi.  Anaefuata ni
Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe  Bw Jesse Kwayu pamoja na wadau
wa Airtel nchini Tanzania 

 Toka shoto ni Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika kitengo maalum cha
mawasiliano Michael Okwiri akipokelewa na Bi. Joyce Luhanga Mkuu wa
Kitengo cha Masoko cha IPP (kati) mara baada ya kuingia katika ofisi
kuu za IPP Mikocheni jijini Dar leo. Mwishoni ni kiongozi wa vipindi
Radio one na Mtangaza wa ITV Bw, Isack Gamba akiwaongoza pia.

Bw, Isack Gamba ambae ni kiongozi wa vipindi Radio one na Mtangaza wa
ITV akiwaelezea jinsi wanavyofanya vipindi na kushirikisha wasilizaji
live katika studio za Radio one sterio jiji dar Mikocheni
Picture Guardian
Bw Wens Mushi ambae ni Kaiumu Naibu Mhariri wa The Guardian akitoa
maelekezo kwa Makamu wa raisi wa Airtel Afrika kitengo cha mawasiliano
(alieshikilia gazeti) huku Bw Alexander Doll Mkurugenzi mkuu wa
Hill+Knowlton Strategies  (wapili toka shoto) toka  kampuni maalum ya
Mahusiano ya Airtel Afrika akifuatilia kwa undani zaidi.  Anaefuata ni
Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe  Bw Jesse Kwayu pamoja na wadau
wa Airtel nchini Tanzania

Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika kitengo cha Mawasiliano atembelea Tanzania
•    Apongeza juhudi za wanahabari nchini Tanzania
•    Ahaidi Airtel itakuwa mstari wa mbele kushirikiana na wanahabari
katika mawasiliano
Makamu wa raisi wa Airtel Afrika katika kitengo maalum cha mawasiliano
kwa umma leo amepongeza juhudi za wanahabari nchini mara ya kutembelea
baadhi ya vyombo vya habari Tanzania ikiwemo IPP media na Mwananchi
Communication ikiwa ni ziara ya siku mbili ya aliyojiwekea ili
kujionea mambo mbalimbali katika ulimwengu wa Habari na Mawasiliano
nchini
Akiongea wakati wa ziara hiyo akiwa na wadau mbalimbali na wanahabari
Makamu wa Raisi wa Airtel Afrika bw, Michael Okwiri alisema
“Nimegundua Tanzania kunamaendeleo mazuri sana hasa ukiangali mitambo
na vyombo vya habari kwa kweli vinaonyesha kupiga hatua kwa kiwango”
Vilevile nawapongeza sana wanahabari (Journalists) kwa juhudi zenu za
kutafuta habari na kuziwahisha kuzichapa kwa muda wa siku pamoja na
mambo mengi, kwa kweli ni juhudi inayohitajika kukamilisha mambo haya
mapema ili wasomaji wapate taarifa inayoendana na muda
Kwa upande wetu Airtel naomba niwashukuru wanahabari wote kwa ujumla
nchini Tanzania hasa mnaoshirikiana nasi Airtel kuhakikisha huduma ya
mawasiliano ya uhakikika inawafikia wananchi kwa kupitia baadhi ya
habari zinazochapwa na kusambazwa nchini na vyombo vyenu.
Airtel tunaahidi ushirikiano wa kutosha katika mawasiliano ili tuweze
kutimiza dhamira yetu ya Uhuru wa kuongea nchini kote” alimaliza kwa
kusezema bw Okwiri

No comments: