22.11.13

Wednesday, March 07, 2012

Airtel Tanzania yadhamiria kuboresha huduma kwa wateja

Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Bi Adriana
Lyamba akiongeaa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake
kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kushoto ni
mkurugenzi Rasilimali watu Perece Kiringiti. 

mkurugenzi Rasilimali watu wa Airtel Tanzania Perece Kiringiti
akiongeaa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programme ya
Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma
bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kushoto ni Mkurugenzi wa
kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba. 

mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Ellangallor akiongeaa na
wafanyakazi wa Airtel wakati uzinduzi wa programme ya Airtel service
Academy  iliyofanyika leo katika Makao makuu ya Airtel Morocco 

Wafanyakazi wa Airtel pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika
uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha
wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
iliyofanyika katika Makao makuu ya Airtel Morocco. 

Keki maalumu ya uzinduzi wa programme ya Airtel Service Academy

Airtel Tanzania yadhamiria kuboresha huduma kwa wateja

*        Watoa huduma 99 kuongezewa ufanisi

*        Katika siku 365
Airtel Tanzania, mtandao unaoongoza kwa gharama nafuu na wenye wigo
mkubwa Tanzania leo umezindua programu ya kuwawezesha wafanyakazi wake
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wateja wake wanapata
huduma bora Tanzania.
Hii  inakuja baada ya ya uzinduzi mzuri wa chuo cha masoko
kilichozinduliwa mwezi wa kumi mwaka jana inayojulikana kama " Airtel
Centum Sales University (ACSU)"
Akiongea katika uzinduzi wa programu hii ya mafunzo kwa  timu
zinazotoa huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel ,Mkurugenzi wa
Airtel Tanzania bwana Sam Elangalloor alisema,"Leo tunazindua rasmi
mafunzo ya huduma kwa wateja Tanzania inayoashiria dhamira yetu katika
kuleta mabadiliko na kuwaopa wateja wetu huduma bora na zenye viwango
vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.lengo letu ni
kuhakikisha tunatoa huduma ambazo zinazidi matarajio ya wateja wetu na
kudumisha mahusiano ya muda mrefu.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa uteja, Adriana Lyamba
aliongeza kwa kusema, " mafunzo haya ni muendelezo wa kuonyesha ni kwa
jinzi gani kampuni na nembo yetu inajali wateja wake.Katika siku 365
zijazo wafanyakazi wa Airtel katika kityengo cha huduma kwa wateja
watajifunza mbinu za kitabia na zile za kikazi katika kutoa ufanisi
zaidi na kuwaongezea ujuzi zaidi.
Leo Tanzania zaidi ya wafanyazi 99 wa kitengo cha huduma kwa wateja
wataanza mafunzo haya ya huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel
makao makuuIn
Programu hii ya  Airtel service Academy inatolewa na kampuni ya
ukufunzi ijulikanayo kama  Centum learning na itahakikisha watoa
huduma wa Airtel wanakua bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.

No comments: