22.11.13

Thursday, March 29, 2012

Airtel yawatangaza washindi wa "Nani Mkali" promosheni

Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi.
Jane  Matinde  akitanzanga washindi wa  promosheni ya Mkali nani kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) ambapo washindi wa siku
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki
hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kulia ni Afisa
mawasiliano wa kampuni ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akishuhudia  tukio
hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini
Dar-es-Salaam. 

Afisa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
Bi. Dangio  Kaniki akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)
wakati wa hafla ya kutangaza washindi wa  promosheni ya Mkali nani
ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja
na washindi wa wiki hujinyakulia kitita cha shilingi milioni
tatu,kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano  wa kampuni ya Airtel Bi. Jane
Matinde akishuhudia  tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni
hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.

 Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa
29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma
nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza
washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo
washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila  mmoja
na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao
wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha,
Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel
Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania
kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa
washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika
promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.  Na leo napenda kuchukua fulsa
hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni
KAANAEL LEMLE KANUYA
ARUSHA
50
1,000,000.00

RAKESH MANSUR DEYAL
ZANZIBAR
34
1,000,000.00

NAPEGWA DAVID MONGO
DSM
58
1,000,000.00

MARIAM WAZIRI HAMISI
DSM
32
1,000,000.00

GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL
ARUSHA
54
1,000,000.00

YUSUPH NOHAI ANNAI
MANYARA
35
1,000,000.00

YUSUPH  MATHIAS MANONI
NZEGA-TABORA
25
3,000,000.00

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha
washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya
kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu
yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio
kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na
kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali
na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo
sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja
na kodi.                                                         

END

No comments: