22.11.13

Sunday, March 25, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - TAMASHA LA MICHEZO

TAMASHA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA SERIKALI YA UINGEREZA NCHINI KUPITIA SHIRIKA LA ‘BRITISH COUNCIL’
TAREHE: 27, MACHI, 2012
MUDA: 4 Asb- 7 Mch
MAHALI: TCC CHANG’OMBE.

UTANGULIZI:
Wizara ya habari, Vijana Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano na Ubalozi wa Uingereza nchini Kupitia shirika la British Council kwa miaka miwili wamekuwa wakiandaa na kuratibu Tamasha kubwa la Michezo linalofanyika mara moja kwa mwaka likiwa na malengo makuu mawili ambayo ni kuhamasisha ushiriki zaidi wa wasichana pamoja na wenye ulemavu katika michezo sambamba na kuwezesha asasi za serikali kushirikiana kwa karibu na wadau pamoja na asasi binafsi zinazojishughulisha na michezo pamoja na maendeleo ya vijana katika kutambulisha na kuonyesha baadhi ya shughuli wanazozifanya katika sekta hiyo nchini.

TAMASHA LA MICHEZO Machi 27, 2012
Kwa mwaka huu wa 2012, Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo kupitia baraza lake linalojishughulisha na michezo nchini ‘Baraza la Michezo la Taifa-BMT’ kwa kushirikiana na shirika la British Council Tanzania pamoja na asasi shiriki za RIGHT TO PLAY, FEMINA HIP, pamoja na GNRC Africa, wamendaa Tamasha la Michezo litakalofanyika siku ya Jumanne ya Tarehe 27, Machi, 2012 katika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saba na robo mchana.
Huku malengo makuu kwa mwaka huu yakiwa ni: Kuainisha na kuenzi mahusiano mazuri baina ya serikali na sekta binafsi katika maendeleo ya michezo. Kuhamasisha sera ya Michezo kwa wote. Kutoa fursa kwa vijana,asasi mbalimbali katika kuonyesha na kubadilishana uzoefu kwenye tasnia ya michezo. Kuadhimisha siku 122 kabla ya kufanyika kwa michezo ya London Olympic 2012. Pamoja na Kutoa fursa kwa wadau mbalimbali kufanya harambee kupitia njia ya kuchangia vifaa vya michezo kwa shule zenye mahitaji maalum.

MAANDALIZI:
Katika hatua za Maandalizi ya Tamasha hili shule za sekondari na msingi zitakazoshiriki zimekuwa zikiendelea kufanya mashindano ya ndani ili kupata timu wawakilishi zitakazo chuana katika michezo ya fainali kwenye michezo ya VOLLEYBALL (Wavulana na Wasichana), MPIRA WA MIGUU (Wasichana), pamoja na RIADHA kuanzia tarehe 21,Machi.
Miongoni mwa shule (3)za sekondari zitakazoshiriki ni pamoja na Kibasila, Azania pamoja na Lord Baden Powell.
Huku Shule za Msingi zikiwa Mbagala kuu, kizuiani, Kibonde maji kutoka wilaya ya Temeke na Ali Hassan Mwinyi, Mwl. Nyerere, Ndugumbi, Mikumi, pamoja na Mzimuni kutoka wilaya ya Kinondoni.
YATAKAYOJIRI KWENYE TAMASHA:
Mbali na kilele cha Michezo ya Fainali kwa michezo ya Volleyball, Mpira wa miguu kwa wasichana na Riadha (Shule za msingi na sekondari).
Pia kutakuwepo na: michezo ya asili na kufurahisha kwa Watoto, Maonyesho ya namna ya kufundisha michezo ya riadha kwa Watoto. Pamoja na Mbio za wazi na kuhamasisha za maili moja kwa wote watakaoshiriki.
MGENI RASMI NA WAGENI WAALIKWA
Katika Tamasha hili Mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi (M)
Pamoja na wageni waalikwa: UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI ASASI MBALIMBALI ZINAZOJISHUGHULISHA NA MAENDELEO YA MICHEZO. VYAMA VYA MICHEZO NCHINI:-
-Chama cha Michezo ya Olympic nchini- TOC
Chama cha Michezo ya Olympic kwa wenye ulemavu- Paralympic-TPC
-Chama cha Mpira wa miguu nchini-TFF
-Chama cha Mpira wa wavu nchini-TAVA
-Chama cha mchezo wa riadha nchini-TAA
Wadau, Wanamichezo, pamoja na wapenzi wote wa michezo mnakaribishwa.
Asante.
Mohammed A.Mvumbagu
KNY Timu ya Waandaaji

No comments: