22.11.13

Thursday, April 12, 2012

Airtel yakabidhi milioni 30 Kwa mshindi wa nani Mkali

 Afisa  uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha
shilingi milioni moja  kwa Camill  Mayo baada ya kuibuka kuwa mshinidi
wa siku na kujishindia shilling milioni moja  katika promosheni Nani
Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka
kuwa washindi.

 Afisa  uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akikabithi kitita cha
shilingi milioni moja kwa Edward Mnewa baada ya kuibuka kuwa mshinidi
wa siku na  kujishindia shilling milioni moja  katika promosheni Nani
Mkali inayoendelea na kuwapatia wateja wa Airtel nafasi ya kuibuka
kuwa washindi.

 Mshindi wa pili wa milioni thelathini wa promosheni ya Nani Mkali
bwana Steven Chapile kutoka Arusha akikabidhiwa kitita hicho na Afisa
uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi
wa pili wa mwenzi wa promosheni ya Nani Mkali inayoendelea na kuwapa
nafasi wateja wa Airtel kujishindia pesa taslimu.

Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki (wa pili kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya nani Mkali
mara baada ya kukabithiwa pesa zao taslimu katika halfa fupi
iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel leo, (wa kwanza
kulia) ni  Camil mayo akifatiwa na Edgar Mnewa waliojishindia milioni
moja kila moja na (wa kwanza kushoto ) ni Steven Chapile
aliyejishindia shilingi milioni 30.

 Wateja wa Airtel kuendelea kujishindia mamilioni

*        Airtel yazawadia zaidi ya milioni 117 bado milioni 100 kushindaniwa
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtanga na kumzawadia
mshindi wa pili wa million 30  wa promoshenii ya Nani Mkali bwana
Steven A Chapile  ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa  Arusha baada
ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya mwenzi na kuzawadia kitita cha
shilingi milioni 30 katika halfa fupi iliyofanyika katika makao makuu
ya Airtel Morocco leo.
Kwa mara nyingine Airtel kupitia promosheni ya Nani Mkali inaendelea
kuzawadia wateja wake na kuwawezesha watanzania kujishindia mamilioni
ya fedha taslimu, mpaka sasa  zaidi ya shillingi milioni 117
zimeshazawadia kwa wateja wanaoshiriki na Kushinda na bado zaidi ya
shilingi million 100 zipo kwaajili ya kuwazawadia wateja
watakaoendelea kushiriki katika promosheni hii ya Nani Mkali.
Katika promosheni hii ya Airtel Nani Mkali  washindi wa siku
wanazawadia shilingi million 1, washindi wa wiki shilingi milioni 3 na
wa mwenzi shilingi  miliioni 30, mbali na kumtangaza mshindi wa
shilingi Milioni 30, Airtel pia imewatangaza na kuwazawadia shilingi
milioni moja kwa washindi 6 wa wiki ambao ni bwana Yunus Lugendo
ambaye ni fundi umeme na mkazi wa babati, Jofrey Shangalawe
mfanyakazi wa Tanesco na mkazi wa Shinyanga, David Samson Njole wa
Mbeya, Denis Mugala  ambaye ni mtumishi wa umma na mkazi wa Rukwa,
Edgar Mnewa na Camil Mayo wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Dar es
salaam.
Promosheni hii bado inaendelea kujiunga na "Nani Mkali", mteja
anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure
kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu
sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe
wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.
Mwisho

No comments: