22.11.13

Thursday, April 26, 2012

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa - Dodoma

Afisa mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi
vitabu vya taaluma bw Leonard Cyprian Ngotta Mwalimu wa taaluma  shule
ya sekondari  Hurui katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya
Sekondari  Gubali  ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu
imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoa
mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma,
Gubali,Itaswi na Hurui, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy
Makamu mkuu wa shule ya Sekendari Gubali

Afisa mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi
vitabu vya taaluma bwana Ibrahim Juma Mwesi Mwalimu mkuu wa shule ya
sekondari Itaswi  katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya
Sekondari  Gubali  ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu
imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoa
mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma,Hurui,
Gubali na Itaswi, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu
mkuu wa shule ya Sekendari Gubali

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa- Dodoma
Chini ya mpango wake wa shule yetu kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari
zilizoko wilaya ya kondoa mkoani Dodoma ili kusaidia maendeleo ya
elimu wilayani hapo na katika kutoa huduma kwa jamii.
Makabithiano hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika
shule ya Sekondari Gubali na shule ya sekondari  zilizonufaika na
msaada huo ni pamoja na  sekondari ya Goma, Gubali,Itaswi na Hurui,
zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa
vitabu vyenye thamani ya shilling milioni moja kwa kila shule.
Akiongea katika hafla ya makabithiano Afisa uhusiano wa Airtel T Afisa
mauzo kanda ya kati bw Hillary Tarimo alisema"  Airtel kwa kupitia
programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule
nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya
shule za sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu
zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na
wanafunzi wa shule zitakazokabithiwa.
Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika
kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu
ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza
Tarimo.
Naye Makamu  mkuu wa shule ya sekondari Galibu Bw Kessy Musilenga
alisema" nachukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kutufikia na kutoa
msaada wa vitabu kwa shule zetu na kupunguza changamoto zilizokuwepo
katika shule hizi, tunayofuraha kwa shule yetu na wenzetu wa shule za
jirani zilizopo wilayani kondoa kupata nyenzo muhimu ambazo zitainua
kiwango cha elimu kwa wakazi na wanafunzi wa wilayani"
Tunawaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo
vizuri kwa wanafunzi, Tunaamini jamii ikipata elimu bora maendeleo ya
shughuli mbalimbali za uchumi yatafanyika kwa ufanisi zaidi na kuleta
mafanikio makubwa kwa jamii. Aliongeza Kessy.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, siku chache zilizopita Airtel
ilitoa msaada wa computer 20 na vitabu vyenye thamani ya million 10
kwa chuo kikuu cha Dodoma - UDOM hii ni katika kurudisha faida
inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.
Mwisho

No comments: