Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania,Man Water (Man Maji),anaendelea na program yake aliyoianzisha ya kutoa zawadi kwa wasanii ambao watakuwa wamerekodi katika studio yake ya COMBINATION SOUNDS,na nyimbo za wasanii hao kuweza kufanya vizuri katika vituo vya redio hapa nchini na nje ya nchi pia.Program hiyo ambayo yeye mwenyewe ameita ni kutoa shukrani kwa wasanii ambao kwa namna moja wanakuwa wanaitangaza studio yake vyema na kumfanya yeye mwenyewe kuweza kujulikana na kupata kazi nyingi zaidi,aliinza kwa msanii 20 percent,ambapo alikuwa ndio msanii wa kwanza kuweza kupewa zawadi na Man water,Kwa kumnunuliwa baadhi ya vyombo vya muziki.
Mwaka huu pia,Man Water tayari ameshatangaza nia yake hiyo ya kutoa zawadi kwa wasanii wawili waliorekodi nyimbo zao katika studio yake ya COMBINATION SOUNDS.Amemtaja msanii wa kwanza kuwa ni ALLY KIBA,msanii ambaye nyimbo yake ya DUSHELELE iliweza kufanya vizuri na kukubalika sana.Dushelele ni nyimbo iliyoweza kufanya vizuri na kushika chati mbalimbali katika radio stations na Tv stations za hapa nchini Tanzania na hata nnje ya nchi.Man Water amemuelezea msanii Ally Kiba kuwa ni msanii mzuri mwenye kipaji na anaamini kwamba ni mmoja kati ya wasanii waliopo nchini Tanzania ambao wanaweza kuufanya muziki huu kuwa bora zaidi na kuutangaza nje ya mipaka ya Tanzania kwa urahisi zaidi.Pia amesema anaamini ataendelea kufanya kazi na msanii huyu ili kuweza kutengeneza nyimbo zenye ubora zaidi na kuendelea kuwaelimisha na kuwaburudisha wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya.
MBATIZAJI,ni msanii wa pili aliyetajwa na Man Water kuweza kupewa zawadi,baada ya nyimbo yake ya HESHIMA KAZI kuweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na television vya hapa nchini.Man Water,amemuelezea Mbatizaji kuwa ni mmoja kati ya wasanii wenye tungo zenye maadili na kufundisha jamii.Amesema mara ya kwanza alikutana na Mbatizaji (kipindi hicho akijulikana kwa jina la MASTA’ BROS) mkoani Morogoro mwaka 2003 na kuweza kusikia nyimbo zake kama “BARUA KWA MAMA” na “NINI MAANA YA MAISHA” na kuona uwezo mkubwa alionao katika utunzi wa nyimbo zake,ndipo mwaka 2005,wakati Man Water akiwa anafanya kazi katika moja ya studio zilizopo mkoani Morogoro,akamrekodia nyimbo iliyojulikana kwa jina la “KIPI HASA?”,nyimbo aliyoipiga ama itengeneza katika midundo ya kapuka(staili toka Uganda).Mwaka jana Mbatizaji aliingia katika studio za COMBINATION SOUNDS na kutaka kurekodi wimbo wa HESHIMA KAZI.Man Water alifurahishwa sana na ujumbe uliopo ndani ya nyimbo hiyo na kummwagia sifa nyingi msanii huyu,ndipo wakati akiwa anamuelekeza MBATIZAJI baadhi ya sehemu,wakajikuta wakiamua kuuimba wimbo huo pamoja ili kuupa radha zaidi na ubora zaidi.
“Unajua ninaufahamu uwezo wa Mbatizaji mda tu,so kwa nyimbo bora kama ile ilinipa hata mimi mzuka wa kuweza kuimba na kurekodi,na naamini hatutoishia katika heshima kazi tu,tuna plan yakuja kufanya kitu tofauti zaidi,kwanza kwa taarifa yako ujue mshkaji nae ni mtayarishaji wa muziki pia,so huwa najisikia kama nafanya kazi na mtu anayefahamu mambo”.Alisema Man Water.
Man Water hakutaka kuweka wazi ni zawadi gani atakazotoa mwaka huu,ila amesema muda utakapofika kutokana na ratiba zake,atawaita wasanii hawa na waandishi wa habari,na kuwakabidhi zawadi hizo.
1 comment:
Master bros au Mbatizaji kwa jina la sasa, aisee man ulipotea sana lkn mimi najua una kipaji kikubwa sana keep it up bro nakumbuka uzinduz wa album yako pale Morogoro Hotel na nyimbo yako moja kama House flan hiv inaitwa sitaweza kukuacha bro umenikumbusha mbali sana BIG UP kaza buti fans wako bado tupo
Its me Haroun
Post a Comment