Majina halisi ni LINET MASIVO MUNYALI a.k.a SIZE 8 kutoka Kenya. Alianza KUIMBA na KUIGIZA akiwa mdogo. Mnamo mwaka 2003 SIZE 8 alijiunga na shule ya upili ya STATE HOUSE GIRLS ambapo alishiriki mashindano ya muziki na UIGIZAJI. Baada ya kumaliza shule mnamo mwaka 2007, SIZE8 alishiriki mashindano ya TUSKER PROJECT FAME lakini hakuweza kuchukuliwa kwa kuwa alikuwa na umri mdogo (Miaka 21) Hata hivyo Producer CLEMO wa CALIF RECORDS aliona kipaji chake na kumsajili kwa studio yake. Baada ya kutamba na nyimbo kama SIZE 8 na SHAMBA BOY dada huyu alijitoa Calif Records na kuanza kujitegemea. Alijiunga na JOMINO RECORDS kwa muda mfupi na kutoa 'CLUB BANGER' kwa jina 'FIRE.' Baadaye aliamua kujitegemea kimziki huku akifanya kazi OGOPA DJs na HOME BOYZ.
Hivi karibuni alishirikiana na ALLY B na kutoa 'another hit' iitwayo SILALI. Mrembo huyu ameamua kuwa hakuna kulala kwani sasa ameachia 'single' yake mpya - VIDONGE - ambayo imekuwa gumzo kila sehemu. Video na wimbo huu wa kuhamasisha na kuchangamsha umetayarishwa OGOPA DJs chini ya producer mahiri LUCAS BIKEDO.
SIZE 8 ndiye msanii wa kike anayetajika zaidi nchini Kenya. Nyimbo zake zote alizotoa zimehit na isitoshe ana mvuto wa kimaumbile na utajiri wa kipaji cha uimbaji. Tazama video za SIZE 8 katika kipindi cha MSETO EAST AFRICA, Citizen TV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia SAA KUMI NA MOJA JIONI (5PM). Afrika Mashariki......mpokeeni SIZE 8 na mpate VIDONGE....
No comments:
Post a Comment