22.11.13

Tuesday, May 29, 2012

HOSPITALI YA TUMBI YAANZA KUPOKEA MSAADA WA MASHUKA

PICHANI: Afisa Uhusiano wa Maxinsure akiongea na waandishi wa habari walipoenda kukabidhi misaada katika hospitali ya Tumbi, kushoto kwake ni Mganga mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Issac Lwari.

Afisa Uhusiano wa Maxinsure akionyesha mashuka alioyakabithi katika hosptali ya Tumbi hivi karibuni.

Meneja Madai wa Kampuni ya Maxinsure ,Bw. Ian Kifunta akishikilia mashuka ya msaada wakati walipokua wanatembelea hospitali ya Tumbi hivi karibuni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk Issach Lwari akiwaonyesha wafanyakazi wa Maxinsure mashine mbovu,iliyokua ikinyooshea nguo za hospitalini hapo.

Hospitali ya Tumbi ya mjini kibaha yapokea msaada wa mashuka 50 yenye thamani ya shillingi za kitanzania 500,000 kutoka katika kampuni ya Bima ya Maxinsure hivi karibuni, Msaada huo ukiwa umetokana na na taaarifa iliyotoka katika gazeti maarufu moja nchini,likiwa linaelezea kuhusu upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.
Kampuni ya Maxinsure ndio imekua kampuni ya kwanza kabisa nchini kuitikia wito huo, huku Bima kuu ya Afya ya nchini ikihahidi kutoa mashuka pia hivi karibuni.
“Tunashukuru sana kampuni ya Maxinsure kwa kuguswa na tatizo letu,tunategemea kupata mashuka zaidi na tunaomba makampuni mengine yaweze kujitokeza kutusaidia, kwani hili sio tatizo pekee linaloikabili hospitali yetu”.Alisema Mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi,Dk.Issach Lwari akishukuru kwa msaada alioupokea
Kwasasa Hospitali ya Tumbi ina mashuka yapatayo 900 huku ikiwa bado na uhitaji wa mashuka yasiopungua 1,124.
DK. Lwari alitaja matatizo mengine kama ,mashine za kufulia, upungufu wa damu na pia hospitali iyo inakabiliwa na ukosefu wa Vipimo mbalimbali ,swala linalopelekea kuwashauri wagonjwa wachukue vipimo katika hospitali nyingine.

No comments: