22.11.13

Thursday, May 31, 2012

MISS UNIVERSE 2011 ‘NELLY KAMWELU’ KUCHANGIA MFUKO WA SARATANI YA MATITI

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu kwa kushirikiana na
Mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer Foundation) wameandaa hafla kwa ajili ya
harambee ya kuchangia mfuko wa saratani ya matiti itakayofanyika tarehe 1/6/2012 siku ya Ijumaa
katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni hadi saa nne usiku.
Vilevile katika hafla hiyo kutakuwa na mnada wa kito cha Tanzanite ambayo imetolewa maalum na
kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya kuchangia mfuko huu. Pia picha ya Mrembo wa Miss
Universe Tanzania itanadiwa katika mnada huo.
Mrembo Nelly Kamwelu toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa akifanya kazi bega
kwa bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo kusaidia kutoa elimu katika shule mbalimbali ili
kupunguza au kutokomeza uwezekano wa kuenea kwa saratani ya matiti. Mfuko huu umepanga
kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Iringa, Mtwara na Lindi.
Kwa kusindikiza hafla hii kutakuwa na maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na wabunifu wa hapahapa
nchini ambao ni Escado Bird, Kemi Kalikawe na Subira Wahure vilevile kutakuwa na burudani ya muziki
kutoka msanii Enika na mchekeshaji Evans Bukuku. Pia mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu atatoa
burudani ya dansi aina ya Belly Dance.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na waandaji wa Miss Universe Tanzania tell: 0714 441165 Mwanakombo
Salim (Mratibu wa Kitaifa)

No comments: