22.11.13

Wednesday, June 13, 2012

ARS National finals

Temeke yaifunga Lindi 4-0 michuano ya ARS.
Timu ya soka ya wanawake wenye umri chini ya miaka 17, imeifunga
wenzao wa Lindi  4-0 kwenye muendelezo wa michuano ya Airtel Rising
Stars uliochezwa jana asubuhi, Jumanne Juni 12.
Magoli ya Temeke yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo
Fatuma Iddi kwenye dakika ya 13 na 19. Arafa Abdul waliwafungia Temeke
goli la tatu huku Niewel Halafan akimalizia kazi kwenye dakika ya 58.
Wakati huo huo, timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya iliifunga timu ya
Arusha mabao 2-1 katika pazia la kufungua mchezo wa fainali Ngazi ya
Taifa ya Vijana chini ya umri wa 17 yanayojulikana kama Airtel Raising
Stars uliofanyika Jumatatu, Juni 11 ya wiki hii kwenye Uwanja wa
Karume ,Dar es Salaam.Huku michuano hiyo ikiwa imetanguliwa na mechi
ya wasichana baina ya Mikoa hiyo miwili huku Mbeya wakisinda 3-2.
Timu ya Arusha ya wavulana walifungua mechi hiyo kwa kasi lakini nguvu
zao hazikuweza kuzaa matunda kabla ya vijana wa Mbeya kufunga goli
dakika ya tisa kupitia mchezaji wake Mussa Msape.Goli hilo  la timu ya
Arusha liliwafanya wachezaji hao kufikiria kutimiza  ndoto zao kuwa
za kweli ambapo  dakika ya 24 mchezaji Shabaaan Jabir wa Arusha
aliwatoka walinda mlango wa Mbeya na kupachika goli hilo.

Ndoto zao zilizimwa kwa goli la ushindi la timu ya Mbeya liliweka
kinywani na mshambuliaji Stanley Kaduma aliyokuwa ni pasi nzuri kutoka
kwa washambuliaji wa mbele. Huku kipindi cha pili kikiwa kimetawaliwa
na pasi na kukosa magoli.
Mbeya wasichana walipata goli lao kwa kwanza dakika ya saba kupitia
mchezaji wake Lucia Venance huku dakika ya 25 Vaileth Mcholuosi
akipachika goli la pili huko la mwisho likiwekwa kinywani na Naomi
Lucas dakika ya 40 huku timu ya Arusha magoli yale yalifungwa dakika
ya 12 kupitia Irine Venance na Venance huyo huyo kupachika goli la
pili dakika ya 27.

Akizungumza wakati wa kufungua nusu fainali za  mashindano hayo ya
wiki moja ,Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano
alisema kuwa Airtel Tanzania wamejikita katika kusaidia na kukuza
mchezo wa mpira wa miguu na kuishukuru serikali pamoja na Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), kwa ushirikiano wake.

Kwa upande wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika kufunfua michuano hiyo aliwataka Makampuni ya simu za mkononi
kuwekeza katika program ya  soka la Vijana. Airtel Raising Stars kwa
mwaka huu iliwashinrikisha shule za sekondari kutoka Mikoa ya Dar e
sSalaam,Arusha, Mbeya na Lindi.
Washindi watatu kutoka kila timu kwenye michuano hiyo watachaguliwa
kujiunga na Klinicki ya kimataifa ya mpira wa miguu itakayofanyika
Nairobi August mwaka huu.
 
End…..

No comments: