22.11.13

Wednesday, June 20, 2012

BIBI BOMBA WATINGA NDANI YA MAISHA CLUB NA KUACHA GUMZO KWA WAGENI WAALIKWA

 Bibi Bomba ni show iliyoanza hivi karibuni na baada ya kuwatafuta mabibi hao wamewekwa wote kwanye jumba la pamoja na mwisho wa shindano atachaguliwa bibi mmoja mkali na aliye Bomba kuwazidi wenzake. Pichani ni msanii wa Bongo Fleva Bob Junior aliwatembelea mabibi hao.

 Babuu wa Kitaa ndio Host wa kipindi hicho cha Bibi Bomba kinachorushwa na Clouds TV pichani akiwa anacheza mziki na mabibi hao.

 Ben Kinyaiya alikuwepo na alifungua shampen kwa mabibi zetu hao

 Hapa bwana hakuna mtu aliamini kama mabibi hao wanajua kuimba vizuri hadi wengine kutumbua mijicho kama ndugu yangu Ben pale hahahaa

safiii

2 comments:

Anonymous said...

tunaelekea wapi sasa, yes tunapaswa tubuni vitu, lakini hii siyo kabisa kutokana na mila na desturi zetu, siyo kila kitu show tu, kama kulikuwa na mpango wa kuwasaidia hao mabibi kivingine siyo kihivyo, binafsi sijapenda kabisa

Anonymous said...

safi sana nimeipenda hiyo ya bibi bomba, wekeni na babu bomba.. watoe stress maana wanakufa kwa mawazo tu