22.11.13

Saturday, July 21, 2012

BODI YA MASHINDANO YAFUTA NA HAITAMBUI MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012

Bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),imefuta na
kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo
fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya
msiba mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya
meli iliyo tokea Zanzibar.
 
Bodi imechukua hatua ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ambalo
limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata uzalendo
kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania Beauty
Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya siku
tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo ya
waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii
Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012
ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine
Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club
Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa
lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es
Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado
point View Pugu.
 
Bodi ya mashindano katiaka kikao chake cha dharula kilichofanyika leo
asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya
uhakika,juu ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua
hatua hiyo kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe
fundisho kwa waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za mashindano haya.
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na
inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu
zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza,
mamlaka za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo
utalii na utamaduni nchini na nje ya nchi.
 
Washiriki wote watalazimika kusubiri tarehe mpya ya kufanyika kwa
shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa
gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za
mashindano zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss
Utalii tanzania wanagharamiwa gharama zote za
mavazi,usafiri,vinywaji,chakula na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili
kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii
kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu anatumia
mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo cha
utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za
Tanzania,tena wakati hata serikali imetangaza maombolezo na bendera
zinapepea nusu mlingoti.
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole Ndugu
zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki,
Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea
wapate kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa.
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha
,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,


Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION (MTTO)

1 comment:

Anonymous said...

Bwana Abubakari Omary Bakari.....Hata Headed Paper hamna!!!!!!!!? Hii si mtu yeyote anaweza kuandika!? Acheni ubabaishaji.....Wekeni logo yenu ndo muweke Tangazo kama hili!!!
JIPANGEE...