22.11.13

Wednesday, July 11, 2012

Vodacom Kutoa Tuzo Kwa waandishi mahiri kumi wa mitandao ya jamii na tovuti Nchini.

·         Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao.
·         Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom
Dar es Salaam, 11 julai, 2012.... Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.
Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii,  Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha  mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
Mwisho.... ///

No comments: