22.11.13

Monday, August 13, 2012

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YAZINDUA UPYA JARIDA LAO LIITWALO “SAUTI YA ILALA”

Ilala municipality is pushing tremendously to promote and publish her social, political and economical manifestation so as to enlighten the beauty, opportunities, talents and the governance of its welfare through different Mediums. This initiative has been propagated by re launching its flagship publication, Sauti ya Ilala, which was previously established in early 2005.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inajitangaza na kujiimarisha katika Nyanja mbalimbali zinazogusa Jamii uchumi sanjari na siasa ndani na nje ya Manispaa hiyo kupitia vyanzo mbalimbali vya habari, kwa kuelewa umuhimu wa habari na haki ya wananchi wake kupashwa habari na kujua mustakabali mzima wa Manispaa yao Mustahiki Meya wa Manispaa hii mh. Jerry SIlaa amezindua upya Jarida la ‘SAUTI YA ILALA”
Jarida hilo ambalo limebuniwa upya na kuongezwa vionjo vipya vya fani na maudhui vitakavyomvutia msomaji kama habari za Manispaa, habari za biashara ndani ya Manispaa, picha za matukio, michezo, burudani na nzuri zaidi muongozo utakao kuwa unaonesha viongozi wote walioko ndani ya Manispaa ya Ilala vyeo na anuani zao kuwezesha wananchi kuwafikia kwa urahisi. Jarida hili limebuniwa upya kuhakikisha linakwenda sambamba na mabadiliko ya kisasa na kumvutia msomaji wa kileo.
Kama msimamizi mkuu na mwezeshaji wa mabadiliko ya Manispaa ya Ialal Mustahiki meya Jerry Silaa anasema’ dhima yake ni kuhakikisha kuwa Ilala inakuwa kitovu cha uchumi wa nchi hii na kufanya maeneo ya katikati ya mji sehemu nzuri, safi na inayovutia na chanzo kikuu cha mapato katika nchi ya Tanzania na maeneo ya jirani. Kwahiyo kupitia Jarida hili watu wataweza kuona shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazofanyika na mafanikio yake.
Akizungumzia Jarida hili pia Afisa uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu anasema Sauti ya Ilala mpya inakwenda kugusa wengi kwa sababu Jarida limebuniwa upya kuweza kukidhi matakwa ya watu wa rika, uchumi, elimu na Nyanja mbalimbali hivyo wananchi watakaopata fursa ya kulisoma Jarida hili watafurahia ladha tofauti.
Katika Manispaa ya Ilala utapata kujionea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na KARIAKOO ambalo ni na soko kuu nchini Tanzania ambapo watu wengi kutoka sehemu mbali mbali za nchi na nje ya nchi jirani hufika eneo hili kwa ajiri ya biashara. Pia Ilala ndio lango kuu la uingizaji na utoaji wa bidhaa nchini kupitia bandari, ikulu, viwanda vikubwa na hoteli kubwa za kisasa ambavyo vyote hivi viko ndani ya Manispaa hii kwa sababu hii basi Jarida hili la Sauti ya Ilala linayo mengi ya kuwaambia wananchi wake na watanzania kwa ujumla juu ya maliasili, fursa, na nini kinaendelea na kutokea ndani ya Manispaa ya ya Ilala .
Katika wakati huu ambapo Teknohama imeshika hatamu “bado tuna dumisha na kuboresha uzuri na uhitaji wa mtu kufurahia kusoma Jarida hili, na zaidi ya hilo jarida hili litakuwa likigawiwa bure na pia litakuwa linapatikana kwenye mtandao na tovuti mbalimbali ambapo litakuwa likitoka mara moja ndani ya miezi miwili.” Alisema Mustafa Hasanali ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya 361 Degrees Inayojihusisha na masuala ya mahusiano ya Jamii, vyombo vya habari na uratibu wa matukio.
Hivyo haja ya kwenda na mabadiliko ya wakati haiishii kwa sauti ya Ilala kuzungumzia masuala ya Ilala tu bali taifa kwa ujumla na ni jukwaa muafaka kwa kujitangaza kibiashara na kufikisha ujumbe kwa hadhira kubwa ya watanzania.
“Sauti ya Ilala, ni Jarida linalotoka mara moja ndani ya miezi miwili linalotoa hali halisi ya Manispaa na tutalitumia Jarida hili kuelimisha, kuburudisha na kuwapasha habari wadau wa maeneo mbali mbali aihitimisha Mustahiki Meya Jerry Silaa wa Manispaa ya ilala’

No comments: