22.11.13

Thursday, August 30, 2012

MUSTAFA HASSANALI TO LAUNCH HIS PINK DESERT COLLECTION AT THE COLOUR IN THE DESERT FASHION WEEK IN BOTSWANA.

Mustafa Hassanali aalikwa kwenye Maonesho ya color in the Desert.

“Pink Desert Collection Toleo la nne la” Hassanali’ mwaka 2012

Mustafa Hassanali kuhamasisha juu ya kansa ya maziwa kupitia mitindo.

Mwanamitindo mkongwe ndani ya Afrika anayetokea Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa katika maonesho ya mitindo ya color in the desert yanayofanyika kuanzia tarehe 31 agost hadi tarehe 1 septemba ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini Botswana katika mji mkuu wa Gaborone.

Akiwa ni mtanzania pekee aliyealikwa katika maonesho hayo ya mavazi yanayosifika Botswana

na Afrika kwa ujumla Hassanali anasema “ Nimefurahi sana na anajisikia fahari na heshima

kuzindua toleo langu jipya la mtindo ikiwa ni la nne ndani ya mwaka huu na nategemea kutumia

fursa hii kuutangaza utamaduni wetu na kuboresha urafiki uliopo kati ya Botswana na Tanzania”.

Toleo hili linaloitwa Pink Desert collection lina magauni yenye alama ya Mustafa Hassanali ikiwa ni pamoja na nguo za kiume ambazo ziko tayari kwa kuvaliwa na kuonesha umaridadi wa mbunifu huyo.

Toleo hili linatoka na kuzinduliwa ikiwa ni kipindi tunachoelekea mwezi oktoba ambao unajulikana duniani kote kuwa ni mwezi wa kuhamasishana dhidi ya ugonjwa wa kansa ya matiti.

‘”Nitatumia toleo hili la mitindo pia katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusiana na tatizo la ugonjwa wa kansa ya matiti ili kila mwanamke aweze kuwa na uelewa wa kujichunguza mwenyewe juu ya afya yake, sambamba na kupenda kuvaa nguo zenye rangi ya pinki kama kiashiria cha uelewa juu ya kansa ya matiti ugonjwa ambao unaathiri wanawake wengi.” Alimalizia Mustafa Hassanali.

Kwa mwaka 2012 Mustafa Hassanali ameshazindua matoleo matatu ya mavazi ambayo ni, Afrikalos aliyoonesha Nchini Nigeria (Lagos), Toleo la Harusi aliloonesha Tanzania (Dar es salaam) na toleo maalumu la mwezi wa Ramadhani liliooneshwa Dakar Senegal.

No comments: