22.11.13

Tuesday, August 28, 2012

USIKU WA SAUTI ndani ya mikoa 4 Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.

Na mwandishi wetu:

KIONGOZI wa zamani wa bendi ya Diamond Sound ‘Dar es Salaam Kibinda Nkoi’, Ibonga Katumbi ‘Jesus’ mwezi ujao ataungana na baadhi ya wanamuziki wengine wa kundi hilo katika onyesho la Usiku wa Sauti na Marafiki wa Kweli litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Martin Kadinda ‘Single Button’ alisema onyesho hilo linahusisha wanamuziki wakongwe ambao wataungana na Jesus pamoja hao wa Diamond.
“Kila kitu kinaenda sawa aliyekuwa amealikwa kwenye onyesho ni Jesus lakini katika onyesho hilo atatakiwa kuimba nyimbo zake kadhaa ambazo alitamba nazo akiwa Diamond na Beta Musica kwa hali hiyo alishauri aite wenzake ili wamsindikize.
“ Kutokana na heshima walijengeana wenzake walikubali kumsindikiza, kwa hiyo mashabiki wa Kibinda Nkoi baada ya miaka 12 wataweza kuwaona tena Ibonga Katumbi, Richard Mangustino, Wayne Zola Ndonga na Alain Mulumba Kashama wakisimama pamoja na kuimba tena nyimbo zao kali,” alisema Kadinda.
Kadinda alisema lengo kubwa la onyesho hilo ni kuthamini muziki wa zamani na kufundisha matumizi ya vyombo vya muziki.
Katika onyesho hilo pia watakuwepo wapiga magitaa kama Elly Chinyama, Adolph Mbinga, Marcis Mengi na mpiga drum wa mwisho kuipigia Diamond Sound Kata Nyama Serikali.
Baadhi ya nyimbo zitakazopigwa katika onyesho hilo ni pamoja na Neema, Mugheni, Chance, Jetou, Bana Beta, Midabwada na Infarouge.  Kadinda alisema wanamuzki wengine watakaoshiriki kwenye onyesho hilo wataendelea kutangazwa.

No comments: