Taarifa
kwa vyombo vya habari
Vodacom
yapunguza gharama za matumizi ya intaneti kwa simu za Blackberry.
Dar
es Salaam, 23, Agosti, 2012 … Wateja wanaotumia
simu za Blackberry sasa watafurahia punguzo kubwa la gharama za matumizi
kutokana na punguzo jpya la vifurushi vya Blackberry (BIS). Kampuni ya simu za
Mkononi ya Vodacom imepunguza gharama mpya za matumizi ambazo zitawewezesha
wateja kupata huduma za Blackberry kwa gharama nafuu kwa wiki na kwa mwezi.
Kwa
wiki mteja atapata huduma za Blackberry kwa shilingi 6000/= pungufu ya gharama
ya awali ya shilingi 7000, Huku mteja atakaejiunga kwa mwezi atalipia 17,500/=
ikiwa ni punguzo kutoka gharama ya awali ya shilingi 20000/= mteja atanunua
vifurushi kwa kupiga *149*01#.
Akizungumzia
punguzo la vifurushi hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania
Rene Meza, alisema kuwa vifurushi hivyo vitakuwa na faida kubwa kwa wateja wa
Vodacom na kurahisisha matumizi ya kila siku ya intaneti kwa wateja.
Huduma
ya intaneti ya Blackberry (BIS) inayojulikana pia kama ‘Blackberry Absolute’
inawawezesha wateja kupata huduma ya intaneti bila kikomo kwa zaidi ya akaunti
nane za barua pepe, Kutuma ujumbe mfupi bila kikomo kupitia (BBM) Blackberry
Messenger Service, huduma za ujumbe mfupi wa maneno kama Live Messenger, Google
talk na Yahoo! Messenger, Blackberry AppWorld na Blackberry Shield, pamoja na
huduma nyingine za taarifa na mawasiliano.
Vifurushi
vipya vya huduma za Blackberry (BIS), vinatarajiwa kuongeza matumizi ya
internet hususani kwa vijana ambao wanatumia intaneti kuperuzi na kupakua vitu
mbalimbali.
Mwisho….//////
No comments:
Post a Comment