Mkufunzi
wa masuala ya aundaaji wa Filamu kutoka taasisis ya Sanaa na uandishi
wa Habari (IAMCO) Ngalimecha Ngahyoma, akizungumza jambo katika Jukwaa
la Sanaa, kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa
na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na kushoto ni Katibu Mtendaji wa
BASATA Ghonche Materego
Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa
nchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze kufanya kazi
zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya
soko la ndani na nje ya nchini.
Akizungumza
katika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu hapa
nchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi katika uandaaji
wa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii kutokuelewa misingi ya
uandaaji wa filamu.
“Kuna maeneo
ya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa utimilifu, na hakuna
njia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana lazima mtu ufundishwe.
Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini matokeo ya kufanya mambo kwa vipaji
ndiyo haya ambayo yanatupa filamu zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,”
alisema.
Alisema ni
muhimu kwa wasanii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuanza kuandaa
kazi kitaalamu ili kufanya kazi zilizobora na kwamba ni vyema kutumia wataalam
katika maeneo yote yanayohitaji utalaam badala ya mtu mmoja kufanya kazi zote.
Kwa upande
wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego,
amesema suala la taaluma alikwepeki katika kutengeneza kazi zenye ubora na
kuwasisitiza wasanii kujiunga na vyuo kupata utaalam katika fani zao.
No comments:
Post a Comment