MSANII
wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria
kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kupitia muziki huku pia akileta
mapinduzi katika sekta hiyo nchini.
Diamond
ambaye ni msanii ghali zaidi kwa sasa Tanzania, amesema kuna watu wengi wenye
vipaji ambao wako mtaani au wako katika sekta nyingine lakini hawajui wafanyeje
ili kufikia ndoto zao jambo ambalo linahitaji watu wengine wawasaidie
kuwafikisha pale wanapotaka.
“Kuna
tatizo ambalo lipo katika mambo ya mitindo, muziki. Watu wengi wanachukulia
kama uhuni, wengi wanaona kama kuuza sura, yaani mtu aonekane kwenye video ili
apate umaarufu, tunatakiwa kubadilisha mawazo haya, Ulaya hata hapo Afrika Kusini
wanaonekana kwenye video wanalipwa.
“Mimi
nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho
wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa
milango kwenye sekta nyingine, wapo wanaoweza kuonekana wanafaa kwenye
matangazo ya biashara, hawa watapata kampuni ambazo zinaweza kuwatumia.
“Katika
majaji watakuwepo Raqey Mohammed wa I-View Studios, hawa wanafanya kazi nyingi
za matangazo, movie, atakuwepo pia Ally Rehmtulah huyu ni mbunifu anaweza
kumuona mtu na akasema huyu anafaa kwa sekta yake, Sammy Cool ni densa na
mwalimu hata Missie Popular yeye ni mwandishi na mwanamitindo wanajua wapi kwa
kuwafikisha watu wengine’ alisema.
Msanii
huyo alisema mafanikio aliyo nayo ya kumiliki nyumba, magari na kujulikana
kwake yametokana na muziki, hivyo ana uhakika wapo watu wengine pia kupitia
yeye na wanamuziki wengine kama yeye wanaweza kufaidika na kufikia mafanikio
kama aliyoyapata.
Diamond
alisema usaili huo unafanyika kesho pale
nyumbani Lounge kuanzia saa tano asubuhi. Hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa
nchini kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaonekana kwenye video yake.
Diamond
pia ndiye msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kuandaa shoo yake mwenyewe
na watu kulipa kiingilio cha sh 50,000. Diamond alifanya hivyo kwenye onyesho
alilolipa jina la Diamond are Forever pale Mlimani City, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment