Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa shindano la Bongo
Star Search (BSS) 2009 Pascal Cassian atazindua albamu yake ya nyimbo za injili
iitwayo Yasamehe Bure kesho (Jumapili hii) katika Uwanja wa Fisi.
Albamu hiyo itakayokuwa na
nyimbo kama vile Chuki ya Nini, Nikumbuke na
Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.
Akizungumzia albamu hiyo
alisema kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa kuwapatia ujumbe wa
neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.
Alisema kuwa akiwa kama kijana ameamua kutumia muda, nguvu na akili zake
nyingi katika kumwimbia na kumsifia Mungu na hivyo ameamua kuwafikishia vijana,
watoto na watu wazima ujumbe kupitia nyimbo.
Pia akizungumzia sababu ya
kuzindulia albam yake katika eneo la uwanja wa Fisi alisema kuwa kutokana na sifa mbaya ya eneo hilo
ameamua ambapo limekuwa likifahamika kama
uwanja wa dhambi kutokana matukio mbalimbali ambayo yanafanyika mahala hapo.
Alisema kuwa mgeni rasmi
anatarajia kuwa Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) Ritha
Paulsen ambae ndie alieibua kipaji chake kupitia shindano hilo mwaka 2009 wakati likiitwa BSS.
Uzinduzi huo pia
utasindikizwa na waimbaji wengine ambao ni Martha Mwaipaja, Sifa John, Joseph
Kaka, Beatrice na wengineo wengi.
Albamu hiyo ambayo
ameirekodia katika studio mbalimbali imemchukua miezi mienne kuiandaa na
itauzwa kwa shilingi 10000/=.
“ Mimi kwanza ninamshukuru
Mungu kwa kuniongoza mpaka kufikia hatua hii ya kuzindua albamu yangu na
ameweza kunifikisha hapa kupitia programu ya BSS ambapo ndipo nilionekana uwezo wangu wa kuimba na kushinda na kumbe
ilikuwa ndio mwanzo wa safari yangu ya kumtumikia Mungu” alisema Cassian
No comments:
Post a Comment