Pichani: Seif Kabelele kutoka http://kabelelejr.blogspot.com/
INANIBIDI NISEME:: Nachukia sana, na inaniuma,
kuona VIJANA ambao ni nguvu kazi ya Taifa wanatumika kunadi itikadi na
sera zenye UFINYU-WA-FIKRA za viongozi vyama vya siasa hapa nchini.. Ni
nani ALIYEWALOGA na KUWADANGANYA kuwa maendeleo na mabadiliko ya kweli
katika nchi huru huletwa kwa KUIITII na KUIPIGANIA RANGI ya BENDERA ya
chama???? Iweje UTUMIKE kukifia CHAMA kuliko NCHI yako???
Miundo mbinu ya nchi haitajengwa na CHAMA. Kamwe maendeleo ya kweli hayaletwi na
VYAMA vya SIASA au UTII kwa Bendera au KAULI-MBIU-POFU zao.. Bali Ni
UONGOZI adilifu, wa WAZI na wenye DHAMIRA ya kuiona KESHO ya TANZANIA
ndio utakaoleta Maendeleo... UKWELI ni kwamba tunaposhindwa kuhoji au
kupima UWAJIBIKAJI na UADABIKAJI wa viongozi tuliowaweka madarakani huwa
TUNARUBUNIWA kuwajadili kwa UPEPO wa KISIASA wa wakati husika.... JAMBO
HILI SI SAHIHI. Yamkini inapaswa kuupitia upya MTAALA wa somo la
URAIA.... Tunapaswa kuiona nguvu yetu kama VIJANA kwa MACHO yote MATATU.
Kama hatuwezi kujifunza kutenganisha kati ya UONGOZI na UTAWALA kamwe
hatutampata anayefaa kuiongoza Tanzania...
2 comments:
Kijana mawazo yako mazuri. Ni kweli watu wanatakiwa kupenda nchi yao na siyo bendela ya chama. Siasa imekuwa kama mchezo wa kuigiza hakuna anayesema ukweli.
Seif Kabelele my Classmet habari za siku nyingi. Tangu tumeachana pale Thaqaafa sec ni muda mrefu. Nakutakia kila la heli .
Mia.... for what u wrote!
Post a Comment