Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Rene Meza akimfafanulia jinsi mkataba
ulivyo wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ,Said Abeid,katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam,wanaoshuhudia wapili toka kushoto Makamu wa kwanza
wa Rais wa TFF, . Athumani Nyamlani,Ofisa Mkuu wa maswala ya Sheria wa
Vodacom Bw.Wallarick Nittu.
Taarifa kwa vyombo vya habari.
Vodacom na TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu.
- Klabu ya Simba Sports Club ndio bingwa mtetezi.
- Msimu wa ligi kuanza Septemba 15, na kushirikisha timu 14.
- Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT ni timu mpya katika ligi.
Dar es Salaam, 11 Septemba, 2012……. Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo limeingia katika mkataba wa
udhamini kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wakati
maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania yakielekea ukingoni.
Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini
wa ligi kuu kwa miaka mitano iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya wa
udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho
hilo kupoea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.
Ligi kuu ya Vodacom itaanza tarehe 15
ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia michezo 182 ikichezwa katika
viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 14, zikiwemo timu za Dar es
Salaam Young Africans, Kagera Sugar na Simba Sports Club ambaye ndie
bingwa mtetetzi wa kombe hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom
Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa kampuni ya Vodacom iko katika mstari
wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na shughuli mbalimbali za
kimichezo ndani ya nchi.
“Wanamichezo wote ni mabalozi wazuri
katika nchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika
kutambua na kukuza vipaji vyao kadri tutakavyo weza,” alisema Meza na
kuongeza kuwa, “Kama jina linavyojulikana ligi kuu ya Vodacom, kombe
hili linashuhudiwa na mashabiki zaidi ya milioni 10 katika mechi 182
zitakazo chezwa sehemu mbalimbali za Tanzania bara.”
Meza amejivunia kampuni hiyo kuwa
wadhmini wa ligi kuu kwa kipindi kingine, na kufafanua kuwa mpira wa
miguu ndio unaongoza kitaifa na unapendwa na Watanzania wengi.
Michuano ya mwaka huu itashuhudia
timu mpya tatu ambazo ni timu ya Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na
Mgambo JKT. Mkataba huu umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya
Vodacom Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kamati
ya ligi.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa
TFF, Athuman Nyamlani, ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania akisema
kuwa anaamini kuwa maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga mkono
vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi.
“Kwa niaba ya TFF, napenda
kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono
mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kuthamini vipaji vya
wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio zaidi,” alisema
Nyamlani.
No comments:
Post a Comment