·
Simu
aina ya Blackberry Curve 8520 kuuzwa kwa shilingi 399,999 na Blackberry Curve
9300 kwa shilingi 599,999 tu.
·
Wateja
watapata huduma za BIS na BBM bure na kifurushi cha kuanzia kwa siku
thelathini.
Dar es Salaam,
3rd September, 2012 … Watanzania walio wengi
sasa watapata uwezo wa kununua simu za Blackberry Smart phone mpya zitakazo
ingizwa sokoni kwa bei nafuu.
Hii inafuatia,
baada ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, kupunguza gharama za
vifurushi vya simu hizo za Blackberry mapema wiki iliyopita. Wateja wa Vodacom
sasa watafurahia ofa mpya ya punguzo la simu hizo kupitia mpango maalum
wa kampuni hiyo wa kurahisisha mawasiliano kwa wateja wake.
Kampeni hii
itahusisha mauzo ya simu aina ya Blackberry Curve 8520 itakayouzwa kwa shilingi
399,999 na Blackberry Curve 9300 ikiuzwa kwa shilingi 599,999. Kupitia ofa hiyo
maalum. wateja wa mtandao wa Vodacom watakao nunua simu hizo watafurahia huduma
mbalimbali za Blackberry kwa siku thelathini mfululizo.
Akizungumzia
mpango huo Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema
kuwa kupitia ofa hiyo wateja watafurahia huduma mbalimbali za Blackberry
Absolute Plan (inayojulikana kama BIS) ikiwa pamoja na matumizi ya BBM
bure, Barua pepe za Blackberry, Blackberry AppWorld, Mitandao ya kijamii ya
facebook na Twitter, foursquare, Linkedln na huduma nyingine za Whatsapp,
Google Chat, akaunti kumi za barua pepe pamoja na Instant Messaging. BlackBerry
Protect na BlackBerry Enterprise Server Express.
“Ofa hii
ya Blackberry itakuwa na manuufaa mengi kwa Watanzania, ninawasihi wateja wetu
waweze kuzinunua na kufurahia huduma mbalimbali kutoka katika simu hizo,”
alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kwa mpango huu nafuu kila mtu anayo
sababu ya kununua simu hizi na kuendelea kufurahia ulimwengu mpya wa maendeleo
ya sayansi na Teknolojia,”
No comments:
Post a Comment