22.11.13

Wednesday, October 17, 2012

PESA HAZITOSHI NEW TISHET IN TOWN

Katika vitu ambavyo nilitamani sana kufanya mwaka huu na mimi kutoa tishet zangu kama wengine wanavyofanya na kuziuza ili na mimi niwepo katika ramani ya watu waliotoaga tishet na watu wakazivaa. 
Kwa hiyo nimeamua kutoa tishet zenye logo ya neno PESA HAZITOSHI ambalo neno hili alinipa baba yangu mzee Mtambachuo mwenyewe na nashukuru kwa kuwa neno hili limebeba ujumbe kibao na mara ya kwanza kunipa neno hili nilifikiria kulifanyia wimbo lakini wakati nafikiria hivyo nikaona hapana ngoja kwanza nianze na tishet kwasababu kuna wasanii wanaoitwa Makomandoo wao wameshatoa wimbo wao unaoitwa PESA AITOSHI so kama idea zimegongana si mbaya ngoja.
Tishet kwa sasa naziuza mwenyewe mwenyewe mpaka pale nitakaposema maduka ambayo nimekubaliana nayo waziuze ndipo nitawaambia, kama unataka kutoa oda ya tishet yako basi wasiliana nami kwa simu namba hii +255 683 164282

No comments: