Ofisa Mkuu wa M-Biashara wa Vodacom Jacques Voogtz
(Katikati) akimuonyesha Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa namna ya kujiunga na
kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa baada ya kuizindua jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza. Kupitia
Faraja bima mteja anweza kulipia bima yake kwa M-pesa.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia
Mtingwa kushoto akimsikiliza jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina
Nkurlu, watatu toka kushoto wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima
kupitia M-pesa,wapili kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom
Tanzania Bw.Salum Mwalim na kulia ni Angela Sompet.
Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa akiongea wakati wa
uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa kwa kushirikiana na
Heritage Insurance,uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa fedha Dk.William Mgimwa akiongozana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza
akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya
Faraja Bima itakayopatika kupitia M-pesa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul
Lewis akisema machache wakati wa uzinduzi huo.
Taarifa kwa vyombo vya
habari.
Watanzania sasa kupata Bima
kupitia huduma ya M–Pesa.
·
Ni ushirikiano kati ya Vodacom na Heritage Tanzania
kuzindua bima ya Faraja, Bima ya mazishi na ajali.
·
Wateja kununua na kulipia Bima kupitia M-Pesa.
·
Huduma ya bure kutolewa kwa wateja watakaolipia huduma
mara kumi kwa Mwezi.
Dar-es salaam, Octoba 3, 2012
… Huduma ya Vodacom ya M-Pesa
imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha Watanzania kufanya malipo yao ya bima
kupitia huduma hiyo.
Hii inafuatia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania
kuzindua Bima ya Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa
kulipwa fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali
ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo ya
kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.
Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza huduma ya vifo
vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao. Ongezeko hili la ziada
litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko dogo la malipo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema wateja wa Vodacom
wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure kwa mwezi.
“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa walau mara 10 kwa Mwezi
watapata bima ya bure ya kiasi cha
Shilingi laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.
Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna haja ya kujaza fomu ili
kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia rahisi kwa kupiga *150*00# na
kuchagua kipengele cha bima. Vodacom inahakikisha kuwa wateja wote wa M-pesa
wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani ndani ya familia zao.
“Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa
zako ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa zako
zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza na kuongeza
kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji na bajeti yako,”
Bima hii ya Faraja
pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza kiwango chake kwa ile yenye
faida zaidi kulingana na mahitaji yao na mabadiliko ya bajeti katika maisha
yao.
Kwa taarifa zaidi
kuhusiana na huduma mteja atapiga 0764 300001 bure au vipeperushi kutoka kwa
wakala wa M-Pesa nchini.
No comments:
Post a Comment