Wapo wanamuziki wa chache wa kike wanaopiga muziki wa kizazi kipya, kwa
sasa, lakini kadri siku sinavyokwenda, wanaendelea kuibuka wanamuziki kadhaa wa
kike ambao kwa hakika wanajitahidi kuziteka nyoyo za wapenzi wa muziki wa
kikazi Kipya.
Mmoja wa wanamuziki hao ambaye ameamua kufunguka na kueleza ya moyoni mara
baada ya kuingia rasmi katika tasnia hii ya muziki wa kizazi kipya ni
mwanamuziki Lady Zhena.
Lady Zhena anaeleza kinagaubaga kuwa ni vyema wanamuziki wa kike nchini
kutambua kuwa, wanapaswa kuwa na moyo wa uvumilivu na kutokata tamaa mapema
kwani hakuna maendeleo ya ghafla na ya haraka.
Anasema wanamuziki wa kike wanapaswa kutilia maanani mazoezi na kujifunza
mbinu za muziki zitakazowawezesha kutunga na kuimba kwa sauti tamu kama wanavyofanya wenzao wanaong’ara hapa Afrika.
Anasema Inafaa pia kwa wanamuziki wetu wa kike kuithamini kazi hiyo kwa
kuiona kuwa sawa na zingine, tena isiyopaswa kuchezewa.
Isiwe tu wanapotoka stejini, basi
wanajiona na kazi ndio imekwisha.
Ni vyema pia kwa wanamuziki wa kike kujiheshimu wakati wote.
Iwapo watajiheshimu wawapo kwenye muziki, ni rahisi pia kwao kuheshimika kwa
mashabiki.
Lady Zhena amefunguka na kusema kuwa
maendeleo ya wanamuziki wa kike na kung’ara kwao kimuziki, kutaamsha
hamasa kwa wanawake wengi wenye vipaji kujitokeza, badala ya ilivyo hivi sasa,
ambapo wengi wanasita kwa kuiona fani hiyo ni ya kihuni.
Mwisho Lady Zhena, anaomba Support kwa watanzania waipokee kazi yake mpya na
kuomba baraka za Watanzania, kwani bila wao yeye si mali kitu.
Single yake mpya aliyoitoa hivi karibuni katika Audio
na Video, aliyomshiriisha B- Baros imeanza kufanya vizuri katika vyombo
mbalimbali vya habari, ikijulikana “Niliteleza” chini ya Usimamizi wa Brabe
Entertainment.
No comments:
Post a Comment