22.11.13

Thursday, January 17, 2013

(Audio) Yard - Nieleze

 Hii inaonyesha ni kiasi gani muziki wa kitanzania unakua kwa kiasi kikubwa, ukikaa chini ukasikiliza track kama hii kwa makini utaona ni jinsi gani tunapanuka kimuziki sasa na kwenda kupiga muziki ambao unatambulika duniani.
     "Nieleze"  iliyopigwa na kijana wa kitanzania anaejulikana kama Yard BASH, imetayarishwa na producer mwenye historia na muziki wa kitanzania, JC (Jesus Christ) anaefanya shughuli zake za muziki MZUKA Records iliyopo maeneo ya Bahari Beach, Dar Es Salaam - Tanzania. “Nieleze” imepigwa kwa miondoko ya "SOUL"  ambao muziki huu unapigwa na wakali wa muziki hapa duniani kama Musiq Soul Child, D'Angelo, BabyFace pamoja na wakina dada kama Alicia Keys na Marehemu AMY WINEHOUSE.
      Muziki huu aina ya"Soul" ni maarufu sana duniani na una wapenzi wengi sana ila Tanzania tulikua tumepitwa kidogo ila sasa naona umeanza kugundulika na watanzania wameamua kuonyesha dhamira ya kuingiza vipaji vyao katika style hii.

     SOUL ni aina ya muziki ambao umetokana na "Gospel" ikiwemo "Rhythm & Blues" (R&B), ambapo SOUL katika society ya BLACK AMERICANS inasimama kama ni Pride na Culture yao.
     Katika miaka ya 1940 mpaka miaka ya 50, Gospel Groups mara chache sana zilikua zinajitambulisha kama aina yao ya muziki ni SOUL. Miaka ya 1960 ndipo ulioanza kusikika huku watu wengine wakiuongelea kama Soul Jazz, maana yake ni Jazz inayosukumwa na maadili ya mapenzi ya kiroho "Jazz Soul" ambapo waimbaji na wataarishaji muziki katika sehemu ambazo wanaishi watu weusi wakaanza kutumia techniques za Gospel Music na ndipo mtindo utambulikanao kama "Soul Music" Ulizaliwa mnamo mwaka 1961.
Sikiliza Na Ku-download hapa chini:  Enjoy!!



Hizi ni lyrics za wimbo huu...

Wimbo: "Nieleze"
Singer: Yard BASH
Producer: JC - [Mzuka Records]

Verse 1: Yard BASH

Amani siiyoni mbele yangu eeehh,
Nahisi nimemkosea mungu wanguu,eh eeh
Ulinitoa gizani ukaniweka mwangani,
Nika-enjoy mapenzi na kusahau ya zamani,
Sasa kuna niniii...
Hii leoooooo...

Chorus:

Ohoooooooo hoooo!!
Baby Nielezeee...!!
Ohoooooooo hoooo!!.......
Hivii imekuajeee ....!! .... x2

Verse 2: Yard BASH

Mimi ni mwepesi kukubali kosa, endapo nimekosa....
Na kama nimekosa...  niambieeeeeee
Natamani urudi... ka zamani, tuishi....
Natamani urudi... ka zamani, tuishi....

Chorus:

Ohoooooooo hoooo!!
Baby Nielezeee...!!
Ohoooooooo hoooo!!.....
Hivii mekuajeee..!! .... x2

Bridge:
Hebu funguka unambie yote yalo moyoni mwakoo…… x2

Chorus:

Ohoooooooo hoooo!!
Baby Nielezeee...!!
Ohoooooooo hoooo!!.....
Hivii mekuajeee..!! .... x2

No comments: