22.11.13

Tuesday, January 08, 2013

HII NI MAALUMU KWA WASANII WOTE MNAONITUMIA NYIMBO MPYA.

Mambo vipi wadau wote wa Bongo Star Link pamoja na wasanii wote wa bongo fleva, leo naomba nizungumze na nyie wasanii mnaochipukia na hata nyie wasanii wakubwa kwa ujumla wasanii wote mnaoimba. 

Mwaka huu 2013 nimeamua kufanya kitu kimoja kizuri tu kama wewe msanii unaechipukia unataka kujulikana kwa watanzania, ningeomba sana pale uunaponitumia wimbo wako hakikisha unakuwa mzuri na sio unakurupuka na kurekodi tu bora mradi umerekodi basi unanitumia ili niweke kwenye blog.

Mwaka huu nitapokea nyimbo ambazo zimetumwa na picha ya msanii aliyeimba na wimbo uwe mzuri hapo nipo radhi kumsaidia mziki wake na sio unatuma wimbo bila picha sasa hapo nakusaidiaje watanzania wakutambue? Nitaziweka kapuni email zote ambazo nitatumiwa wimbo bila picha nzuri ambayo ina ukubwa na sio kipicha kidogooooo hata kwaliti yake haifai kukaa kwenye blog.

Wasanii wakubwa unaponitumia wimbo kuwa basi kimataifa sio unanitumia wimbo ukijua wewe msanii mkubwa basi nitakuwa na picha yako, wengine inanipasa hadi kuingia Google ndio nipate picha yake. Piga picha nzuri ili watu wakuone kimwonekano wa sasa hivi kama ulivyotoa wimbo mpya basi tuma na picha mpya.

Email ya kutuma nyimbo zenu kuanzia sasa ni hii djchoka84@yahoo.com

Nawatakia heri ya mwaka mpya na mungu atujalie tuende nao vizuri na mabadiliko yatokee japo kidogo kwenye Bongo fleva na sio kuwa vile vile tu hakuna mabadiliko.

It's me
DJ CHOKA aka Mr. Appetite aka Baba Harrison

Facebook Fans Page: DJ CHOKA
Instagram: DJCHOKA
Twitter: ChokaDJ
Skype: djchoka1
Youtube: 84Choka
Soundcloud: djchoka
Hulkshare: Hugoline
WhatsApp: +255 683 164282

No comments: