22.11.13

Tuesday, January 08, 2013

Sijaibiwa Mil 7 Jamani huu ni UZUSHI "TUNDA MAN"

Msanii Tunda Man anayeipeperusha bendera ya TIP TOP ameongea na DJ CHOKA kwamba kuna story inazagaa kwenye mitandao ya jamii na baadhi ya Blogs kwa ameibiwa Mil 7 na jimama. Habari hizo si za kweli na Tunda amekasirika sana anashangaa kwanini watu wanavumisha habari hizo? Namnukuu

"Hizi habari si zakweli Choka, unajua mambo mengine hata mzazi wako anaposikia habari zakuibiwa hela sijui na jimama wakati yeye anashida na hela anakuwa hala amani tena na wewe kwasababu unaweza kukuta alikuomba kiasi kidogo lakini wewe ulimpiga chenga ili ujipange zaidi halafu mtu anakuja kusema nimeibiwa Mil 7 na jimama wakati hata hizo hela sina kwa wakati mmoja" 

So Tunda Man anawaomba mashabiki wake wasichukulie habari kwa juu juu tu bila kutafuta ukweli uko wapi kwanza anasema ni maadui zake ambao hawapendi maendeleo na mziki wake ndio waliovumisha hivi habari bila sababu.

1 comment:

Anonymous said...

GOOD KAMA SIO M7? NI KWELI ALIIBIWA NA JIMAMA? MANA NAONA AMEKANUSHA KITU KIMOJA TU, KUIBIWA M7 NA JIMAMA, CHA KWANZA ALIPASWA KUSEMA KAMA NI KWELI KUNA JIMAMA LILIMTAPELI, KWA HIYO TUNDA JIMAMA LIMEKUIBIA BEI GANI?