ONE
BILLION RISING: Dar es Salaam
Dar es Salaam INAJIUNGA NA KAMPENI YA
ULIMWENGU - ONE BILLION RISING - KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA
WASICHANA
Tarehe 14 Februari, 2013 kuwa Siku
Kubwa Kabisa ya V-Day Ambayo haijawahi kutokea
Dar es Salaam
INAJIUNGA NA KAMPENI YA ULIMWENGU - ONE BILLION RISING - KUKOMESHA UKATILI
DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA
Tarehe 14
Februari, 2013 kuwa Siku Kubwa Kabisa ya V-Day Ambayo haijawahi kutokea
Dar es Salaam: Tarehe 14, Februari,
2013, saa 10 jioni, Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati duniani kote kwa
ajili ya ONE BILLION RISING, siku kubwa kabisa ya utekelezaji katika historia
ya V-Day, harakatiza wahamasishaji kimataifa kukomesha ukatili dhidi ya
wanawake na wasichana.
ONE BILLION RISING ilianza kama wito wa
kuchukua hatua kutokana na takwimu ya kushtua kwamba mwanamke 1 kati ya 3
duniani atapigwa au kubakwa wakati wa uhai wake. Kwa kuwa idadi ya watu duniani
imefikia bilioni 7, hii inamaanisha zaidi ya WANAWAKE NA WASICHANA BILIONI
MOJA. Tarehe 14 Februari, 2013, siku ya maadhimisho ya miaka 15 ya V-Day, Dar
es Salaam itajiunga na wanaharakati, waandishi, wanafalsafa, watu mashuhuri, na
wanawake na wanaume duniani kote tutakapoeleza hasira zao, kudai mabadiliko,
kugoma, kucheza, na KUAMKA ili kupingana na mateso ya uonevu wayapatayo
wanawake, hatimaye kudai kukomeshwa kwa ukatili dhidi ya wanawake.
"Tulipoanza V-Day miaka 14
iliyopita, tulikuwa na wazo lisilofaa kabisa kwamba tungeweza kukomesha ukatili
dhidi ya wanawake," alisema Ensler. "Sasa, tunastushwa na hali
kadhalika kufurahishwa kuona kwamba hatua hii ya kimataifa inakua na kupata
nguvu, na wafanyakazi, wabunge, watu mashuhuri, na wanawake wa asili zote
wanajiunga na kampeni hii. Tutakaposhirikiana hapo tarehe 14 Februari, 2013
kudai kutokomezwa kwa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana itakuwa sauti ya
kweli ya kimataifa itakayokomesha hali hii. "
Tuamke Dar itafanyika
Coco Beach, Oysterbay siku ya Alhamisi, tarehe 14 February, 2013 saa 10 jioni.
Kutakuwa na muziki na kucheza, hivyo tunawaalika wake kwa waume kuja kujumuika
nasi na kuamka na kuinuka pamoja kukemea ukatili dhidi ya wanawake.
No comments:
Post a Comment