Wednesday, February 13, 2013

ONE BILLION RISING: Dar es Salaam

ONE BILLION RISING:  Dar es Salaam

Dar es Salaam INAJIUNGA NA KAMPENI YA ULIMWENGU - ONE BILLION RISING  - KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA

Tarehe 14 Februari, 2013 kuwa Siku Kubwa Kabisa ya V-Day Ambayo haijawahi kutokea

Dar es Salaam INAJIUNGA NA KAMPENI YA ULIMWENGU - ONE BILLION RISING - KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA
Tarehe 14 Februari, 2013 kuwa Siku Kubwa Kabisa ya V-Day Ambayo haijawahi kutokea
Dar es Salaam: Tarehe 14, Februari, 2013, saa 10 jioni, Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati duniani kote kwa ajili ya ONE BILLION RISING, siku kubwa kabisa ya utekelezaji katika historia ya V-Day, harakatiza wahamasishaji kimataifa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
ONE BILLION RISING ilianza kama wito wa kuchukua hatua kutokana na takwimu ya kushtua kwamba mwanamke 1 kati ya 3 duniani atapigwa au kubakwa wakati wa uhai wake. Kwa kuwa idadi ya watu duniani imefikia bilioni 7, hii inamaanisha zaidi ya WANAWAKE NA WASICHANA BILIONI MOJA. Tarehe 14 Februari, 2013, siku ya maadhimisho ya miaka 15 ya V-Day, Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati, waandishi, wanafalsafa, watu mashuhuri, na wanawake na wanaume duniani kote tutakapoeleza hasira zao, kudai mabadiliko, kugoma, kucheza, na KUAMKA ili kupingana na mateso ya uonevu wayapatayo wanawake, hatimaye kudai kukomeshwa kwa ukatili dhidi ya wanawake.
"Tulipoanza V-Day miaka 14 iliyopita, tulikuwa na wazo lisilofaa kabisa kwamba tungeweza kukomesha ukatili dhidi ya wanawake," alisema Ensler. "Sasa, tunastushwa na hali kadhalika kufurahishwa kuona kwamba hatua hii ya kimataifa inakua na kupata nguvu, na wafanyakazi, wabunge, watu mashuhuri, na wanawake wa asili zote wanajiunga na kampeni hii. Tutakaposhirikiana hapo tarehe 14 Februari, 2013 kudai kutokomezwa kwa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana itakuwa sauti ya kweli ya kimataifa itakayokomesha hali hii. "
Tuamke Dar itafanyika Coco Beach, Oysterbay siku ya Alhamisi, tarehe 14 February, 2013 saa 10 jioni. Kutakuwa na muziki na kucheza, hivyo tunawaalika wake kwa waume kuja kujumuika nasi na kuamka na kuinuka pamoja kukemea ukatili dhidi ya wanawake.

No comments:

Post a Comment