Kushoto Phabian Duwe Mkurugenzi wa Tanzania Msic Power, Evelyn Munisi meneja TMP, Ludovic K Mugasha
KAMPUNI YA TANZANIA MUSIC POWER ENTERTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM IKISHIRIKIANA NA HOTEL DEMAGYA MWANANYAMALA DSM, IMEANDAA TUZO KWA WAPENDANAO KWA MWAKA 2013 IKIWA NI KWA MARA YA KWANZA KUFANYIKA TUZO KAMA HII HAPA NCHINI AMBAPO KWA MWAKA HUU WAPENDANAO WAWILI AMBAO NI MFANO WA KUIGWA KATIKA JAMII KATIKA KUDUMU KWAO KATIKA MAPENZI KWA KUVUMILIANA NA HADI KUFIKIA MAENDELEO AMBAPO PIA WAMEWEZA KWA PAMOJA MAFANIKIO WALIYOYAPATA KURUDISHA KWA JAMII KWA NJIA MBALIMBALI IKIWEMO KUTOA AJIRA AU MCHANGO MBALIMBALI KWA WAHITAJI.
KUTOKANA NA HILO KAMPUNI YA TANZANIA MUSIC POWER ENTERTAINMENT IMEONA UMUHIMU WA KUMZAWADIA TUZO WAPENZI WA NAMNA HIYO KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA JAMII NA KUDUMU KATIKA MAHUSIANO KWA MUDA MREFU BILA MFARAKANO AMBAO ULIONEKANA WAZI HADI KATIKA JAMII.KUTOKANA NA HAYO KAMPUNI HIYO ITATOA TUZO HIYO YA THE BEST COUPLE 2013 KWA MTU YEYOTE KATIKA JAMII YETU BILA KUJALI ITIKADI YAKE ANAWEZA KUWA MBUNGE,MSANII WA BONGO FLAVA,MSANII WA BONGO MOVIE,WAZIRI KATIKA BARAZA LETU LA MAWAZIRI AU MTU YEYOTE MAARUFU KATIKA JAMII INAYOTUZUNGUKA.MSHINDI WA TUZO HIYO ATAPATIKANA KUPITIA TAFITI ZETU KATIKA VYOMBO VYA HABARI MBALIMBALI,MAGAZETI,RUNINGA, RADIO,MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII N.K AMBAYE KIMSINGI MSHINDI WA TUZO HIYO SHARTI ANATAKIWA AWE AJARIPOTIWA VIBAYA AU KUWA NA SKENDO MBALIMBALI ZINAZOMCHAFUA.
TUKIO HILO LITAFANYIKA SIKU YA WAPENDANAO AMBAYO ITAKUWA NI ALHAMISI IJAYO YA TAREHE 14FEB 2013 KATIKA HOTEL YA DEMAG ILIYOPO MWANANYAMALA KOMAKOMA DAR ES SALAAM AMBAPO PIA KUTAKUWA NA KIINGILIO, WAPENDANAO WAWILI( VALENTINE COUPLES) SH.70,000/= AMBAYO ITAJUMUISHWA NA BUFEE ,VINYWAJI,KUOGELEA NA COACK TAIL.NA SINGLE SH,50,000/= ITAJUMUISHWA HUDUMA HIZO ZA KWANZA AMBAPO PIA KUTAKUWA PIA NA BURUDANI YA MUZIKI WA LIVE,MWANAMUZIKI RODGERS LUCAS AMBAYE MSHINDI WA PILI KATIKA SHINDANO LA BSS 2011 ATATOA BURUDANI YA UHAKIKA KUPITIA GITAA LAKE LIVE NA VILEVILE KUTAKUWA NA SURPRISE KIBAO ZA BURUDANI NA ZAWADI.
KARIBUNI………
No comments:
Post a Comment