Mida ya saa kumi
nilitoka kwenda tizi kwa maana hua nachezaga basketball, nikafunga studio
vizuri nikaenda kwenye kikapu kurudi mida ya saa moja kasoro saa kumi na mbili
hivi nimefika tu mlangoni nikakuta mlango upo wazi kabisa nikajua hapatayari
wamefanya yao wezi nikaingia ndanikukagua kama wamesafisha studio nzima au
wamenisamehe vingine ndo nikagundua wezi wameiba vitu vya kubebeka fasta fasta
kama Laptop aina ya gateway touch screen, head4n za studio,speaker pamoja na
external ilikua pia pale juu.Vitu vyote hivo vinagarim zaidi ya milion 1,na
extenal waliobeba ilikua na kazi za wasanii za kutoka this february lkn leo
asubuhio nimepata backup ingine japo sio data nyingi.
Kazi zilizoenda na maji ni
kama kazi ya Chiddi Benz, Peter Msechu, Noorah na nyingine nyingi tu, nimeshatoa
taarifa polisi na wanashughulikia hilo simuhisi mtu yeyote yule kwa sababu sina
ugomvi na mtu yeyote yule
No comments:
Post a Comment