Mimi Abdul-Aziz Abubakari Chende ninae
julikana kwasasa kama Janjaro ninaandika ujumbe huu uwaaendee waTanzania
wote Mimi ni kijana Mwenye Umri Wa Zaidi ya Miaka 18 Ninasoma Shule Ya
Makongo Kidato Cha tatu Baada ya Kuwa nimefaulu Kidato Cha pili Pia Vile
Vile ninajihusisha na Kazi ya MZIKI" nikiwa katika Lebo ya MTANASHATI
ENTERTIANMENT Chini ya OSTAZ JUMA NAMUSOMA....
ninayatoa YA MOYONI Kazi
yangu ya Mziki Ndio iliyofanya
kila Mtanzania kunitambua kama mimi JANJARO nanikajizolea Mashabiki
Wengi hivyo na kila Mtanzania kunitambua kama ABDUL-AZIZ au JANJARO nina
Talent (KIPAJI) lakini sasa kipaji Icho kilitokea nikiwa na umri Mdogo
ikiwa ninaSoma hivyo nlitokea kukipenda sana kipaji changu na
kukithamini sana kwani ndicho kilichofanya kila mtanzania kunitambua na
pia mziki huo huo uliweza kusababisha mimi kuonana na viongozi Wakubwa
Wakubwa katika Serikali Mojawapo Akiwa MH RAIS WETU WA JAMUHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA...JAKAYA MRISHO KIKWETE amenitambua mimi kama
JANJARO sababu ya MZIKI
kwahiyo nitauheshimu mziki na kuupenda na
kuendelea kuthamini kwa sababu umenifikisha mbali MACHUNGU yananiingia
MOYONI nakunifanya KUWA MNYONGE kwa Baadhi ya WATANZANIA Ambao hawapendi
Maendeleo yangu na Mafanikio yangu kutumia Shule ni Kigezo cha
Kuniponda,kuniDhalilisha,kunit ukana,na
baadhi ya Watu wengine Wenye mitandao kama WebSite au Blog na
Facebook,Kuandika habari Zisizo kuwa na Uchunguzi na Uhakika Kwakua ni
wavivu wa kutafuta habari wakikurupuka tu kitandani wanaandika JANJARO
kafukuzwa Shule Mara Janjaro Kafeli Mara Janjaro kaacha Shule ikiwa sasa
Hawawezi kuiendesha Mitandao yao katika habari za Uhakika waache
Wasijihusishe na kazi za habari nakumbuka nikiwa katika Tour yangu ya
South Africa MILLARD AYO Alifanikiwa kunipigia Cm nikiwa Nje ya Tanzania
anaefanya kazi katika Ofisi ya CLOUDS MEDIA GROUP alinipigia cm na
kunifanyia Mahojiano kwahiyo nilifurah sana nikaona anaithamini kazi
yake hapendi kutangaza kitu kisichokuwa na uhakika ANAPITA Anaefanya
kazi katika EA RADIO kipindi cha POWE JAMES tunachat na kuwasiliana
katika BBM pia Huwa Atangazi kitu bila kuniuliza na DJ CHOKA MR APPETITE
pia aweki kitu kwa Blog yake bila kuniuliza hawa ndio nliokua
nikiwasiliana nao nikiwa Safari,
Tafauti na Hao, watakaoandika habari
Totauti isiyofanana na hao nnaowasiliana nao juweni hao ni waongo ni
wavivu wa kutafuta habari Wasiwapotoshe Watanzania ninaOmba kuzungumza
Neno la mwisho.. Mimi Abdul-Aziz Abubakari Chende Ninae julikana kwa
jina la JANJARO SIJAFUKUZWA SHULE,WALA SIJAACHA SHULE,NAWALA SIJAFELI na
NIPO KIDATO CHa TATU...Form III ndio DARASA LANGU NA NDIO MAANA
NIMEWEZA KUANDIKA NYIMBO YA MAISHA YA SKONGA na Najua itamgusa Kila
Mwanafunzi ,Ikiwa Safari yangu ya Kwenda SOUTH AFRICA IMEWAUMA BASI
FAHAMUNI YA KWAMBA nimejifunza MENGI katika SAFARI YANGU
Kwanza
imenifanya nizidi kujua mziki zaidi pili imenifanya nijue kufanya show
za kiInternational tatu imenifanya nikutane na Mastar wengi wakanifahamu
tukabadilishana Contact.. Wakasikiza kazi zangu na kuwa na Connection
nao hivyo naomba mtambue mziki pia ni moja ya Maisha yangu ni kama vile
nna miguu miwili shule mguu wa kwanza mziki mguu wa pili hivyo siwez
kukata wowote katika iyo miguu miwili... AMEEN..napenda Shule napenda
mziki,Narudia tena Napenda Shule napenda mzik...NAMSHUKURU MUNGU KWA
KUNISAIDIA KUFIKA HAPA.. Naishukuru COMPANY YANGU YA MTANASHATI/OSTAZ
JUMA.../Nawapenda WATANZANIA
No comments:
Post a Comment