Kina dada watatu kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania, The
TRIO, wametoa wimbo wao mpya unaoitwa, ‘PAMBO’ ambao ni maalumu kwa ajili ya
kuadhimisha siku ya wanawake duaniani.
Kundi hilo ambalo limekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu
kidogo, sasa wameamua kutoa wimbo huo ikiwa ni maandalizi ya ujio wao kamili
mwishoni mwa mwezi huu.
Pamoja na wimbo huo, The TRIO pia wametoa video ya live
performance ya wimbo wao wa ‘FALL IN LOVE’ ambayo ilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye
vituo vya luninga wakati wa sherehe za Valentine mwaka huu.
Kundi hilo linaundwa na kinadada watatu machachari, Angella
Karashani (Malaika), Alice Kibopile (Alice) na Khadija Maige (Kadja)
Wimbo umerekodiwa studio ya Sourround Sound, chini ya
mtayarishaji Ema The Boy.
No comments:
Post a Comment