22.11.13

Friday, April 19, 2013

(Advertising) MIAKA 13 YA LADY JAYDEE NA UTAMBULISHO RASMI WA ALBUM YA "NOTHING BUT THE TRUTH" - SOKONI

Mwaka huu narudi tena kuadhimisha miaka 13 ya
Lady JayDee, With a New Team.

Nawaletea fans wangu Album yangu ya 6
Inaitwa "Nothing But The Truth"

Ina Jumla ya nyimbo 10, na zote ni ukweli wa maisha ya kila siku yanayoendelea humu duniani tunamoishi.
Single ya kwanza mmeisikia, na ninashukuru mmeipokea kwa mikono miwili

JOTO HASIRA
Na mimi nasema Amen
Tanzania niwape nini tena zaidi ya Shukrani?
Mmekuwa mkinibeba siku zote. 


Nawapa dodosa tu ya yanayokuja, tarehe?, siku? muda? na mahala? nitawafahamisha punde kila kitu kikikaa kwenye mstari.
Mbali na Lady JayDee kutakuwa na wasanii wengine wakubwa watakaoshiriki katika show hiyo kubwa ya kihistoria.

Endeleeni kutegea sikio vituo mbalimbali vya radio kama
East Africa Radio, Magic FM, Times Fm
Na television zingine kama EATV, Channel ten na Star TV.
Ili kufahamu nini kinakuja kwenye show hii

Familia ya pili yani LA FAMILLE 2
Itaundwa kabla ya show hii ya miaka 13 ya JayDee
Na wote watapata fursa ya kuhudhuria show zote Dar na Mikoani, pindi wapatapo nafasi.

Tayari wamekwisha patikana members 6 bado 14 kutimiza idadi ya 20.
Famille inatakiwa kuwa na watu 20 tu.
Do u wana be one of them??? Kazi kwako

Kutakuwa na dinner ya pamoja na La Famille 2
Wiki mbili kabla ya show kubwa kufanyika

Na mwisho
Nashukuru na radio zooote za mikoa yote ya Tanzania mlioipokea Joto Hasira, kuwataja mmoja mmoja naweza shindwa ila habari nimezipata na ninasema hiviiii
Mapenzi tele kwenu nyote

With Lots of Love n Respect to you all.
Komando JIDE
a.k.a
ANACONDA

No comments: