22.11.13

Tuesday, April 09, 2013

(News) HIVI NDIVYO VIGEZO VYAKUTUMA NYIMBO KWA SASA DJCHOKAblog

Habari
Leo naomba kuzungumza na wasanii wanaonitumia nyimbo zao wakitaka nizipandishe kwenye blog hii, naomba niseme hivi kuanzia leo DJCHOKAblog itapandisha zile nyimbo kali tu ambazo zitakuwa zimeendana na vigezo na masharti kutoka kwangu. 

Vigezo hivyo ni kama msanii mkali anayeimba vitu vyakueleweka kwa jamii nikimaanisha sio anaimba maneno yenye lugha chafu, wimbo uwe umefanyiwa mixing nzuri na sio kukurupuka na kutuma wimbo bora mradi sauti yako imesikika, wimbo utumwe katika format ya MP3 na nyimbo nazopokea ni zile zinazotumwa kwenye email tu na sipokei wimbo usiokuwa na picha ya msanii na picha iwe nzuri.

Kuna kitu ambacho sijakipenda natumiwa nyimbo nyingi sana kupitia account yangu ya Facebook, WhatsApp na BBM, jamani naomba nirudie tena sipokei wimbo au nyimbo kupitia inbox yangu ya Facebook, WhatsApp wala BBM. Nilitoa namba ya WhatsApp na Pin ya BBM ili tu kwaajili ya kuchat na kubadilishana mawazo. 

Nyimbo zote pamoja na picha ya msanii aliyeimba na pamoja na link ya video kama uliweka Youtube zitumwe kupitia email hii tu djchoka84@yahoo.com na sio kwingine, nitakuwa napandisha nyimbo kwa blog zile ngoma kali tu kwa maana napata malalamiko naweka nyimbo mbaya bora mradi umeitwa wimbo basi niweke tu hewani.

Nashukuru kama nimeeleweka kwa kila msanii ambaye anaipenda kazi yake hata nyie wakubwa pia angalieni kazi zenu sitokuwa na upendeleo kama kweli tunataka mziki wetu ufike pale juu na sio kubaki katikati.

NITAKUWA MKALI KIDOGO SAFARI HII ILI NIELEWEKE VIZURI.


Follow Me:
Twitter: @ChokaDJ
Instagram: @Chokadj & @bongostarlink
Facebook Page: DJ CHOKA
Skype: djchoka1
Kik: Chokadj
Viber: +255 683 164282
WhatsApp: +255 683 164282
BBM: 286218EE

5 comments:

nestory said...

kweli bro Dj choka hiyo poa sanaaaa iki kukuza muzk indstry ya Tz daaah God bless u bro inafanya poa sanaaa mana bongo Artist wanaimba ilimradi mpaka wanakeraaa..... From N njau

EDDYDEWITTY said...

hapo pazuri kozi wasanii hawajitambui

hammy mohamed said...

kiukweli hii me nmeipenda sana hasa pale dj choka aliposema.....
Ngoma kama haiko kwa maadili yaan kwa iko kwa maneno mabovu, hata kama msanii mkubwa huipokei pamoja sana ma bro!!!!

Anonymous said...

Choka,

We this is the second time una weka hii. VERY VERY GOOD.

Naomba Ongeza Hili kuwa wasanii wawe namba zao za simu, there is something i want to start using your Blog.

I will send you more details for you and others support.

Nirijaribu kutuma maelezo kwa baadhi ya blogs and Gov't entities, ya jinsi mssanii mmoja anavyoweza kutengeneza 50,000,000 na serikali kuweza kutengeneza zaidi ya 50,000,000 for a Single Track - ila naona responce ni ndogo, with you and others support, naamini tutafika somewhere, sehemu ambayo wasanii hawatokuwa watumwa wa kazi zao wenyewe wala hawatotegema ku-hit ili kufanikiwa.

Merci,

Prince SAB.

Anonymous said...

Iko poa sana, labda itapunguza ukiukaji wa maadili kwa wasanii.

Ila siku hizi kwenye hulkshare hamna option ya download kwa ku2mia simu. Help please dj!!