22.11.13

Tuesday, May 07, 2013

(Lyrics) Kala Jeremiah - PASAKA

wimbo PASAKA
msanii KALA JEREMIAH
album PASAKA

nI ASUBUHI YA PASAKA MCHIZI NAITUPA SHUKA
DA! NIMEJISAHAU KUMBE KUMESHAPAMBAZUKA
OK MZUKA NACHUKUA MSWAKI FASTA BAFUNI NAIBUKA
BILA KUJIREMBA BILA KUTAMBAA DAKIKA
NAJIPIGA WESE KISHA NA PAMBA NANYUKA
OK NGOJA NIENDE KWA YULE DEM WANGU MUUZA DUKA
NIKAMSET ANITOE NIKAJILIPUE NA VODKA
HAINA USAKA,MWENDO HATUA KADHAA NAWAKUTA MAKACHAA WANAMFANYIZIA KIBAKA

MASELA mwizi huyo mwizi huyo mwiziiiiiiii
MWIZI jamani siyo mimiiiiiiiiiiiiii

SISHANGAI KWETU ISHAZOELEKA
DAILY FUJO DAILY WIZI NA MAAFANDE WASHATUCHOKA
OK ULE NDO MLANGO WA DUKA NGOJA NISOGEE KARIBU NIONE VIPI NITACHEKA?
MARA GHAFLA MAMBO YANABADILIKA
MAJAMBAZI WANAVAMIA KWENYE LILELILE DUKA
RISASI ZINATUMIKA PILIKA JUU YA PILIKA
WATU WANATOWANYIKA

(milio ya risasi)
JAMBAZI woote kaa chini nitawatifua ubongo shit!

NAJIKATAA MITAA YA NYUMA RISASI MITHILI YA VITA
NYUMA NASIKIA BADO ZINAMIMINIKA
NAJIKWAA NADONDOKA NANYANYUKA
NDUKI,NASHUKA BONDENI NINAWAKUTA MAJITA
ZIKO MCHIZI KAMA SITA DOGO MMOJA NA MASISTER
NINAWAPA HI WALE MAJITA WANANIITA
KUWAFUATA KAMA KAWA SI NIKAKUTA WANAVUTA

MVUTA BANGI oyaaaa mwana mbona lesi sana au ndo ujana nini eeee?

MIMI ujana wapi ndugu yangu we acha tu yaani leo tokea asubuhi misala juu ya misala kwanza nitembezeee kitu hicho

DOGO oyaa maafande

AMA KWELI SIKU YA KUFA NYANI MITI HUTEREZA
GHAFLA BIN VUUU MAAFANDE WAKATOKEZA
KILA MTU NJIA YAKE SPIDI YAKE DU! BABAKE
MSHIKE MSHIKE KAMA NDEGE KWENYE TUNDU
MARA MAAFANDE WAKASIZI NIKAWAZIDIA UTUNDU
BREKI YA KWANZA GETO NIKAFIKA NIKALALA
USINGIZI MASAA MA NANE NIKAOTA NDOTO YA KAFARA
NIKAOTA NIMECHINJWA NIMEKUFA NIMETUPWA NA OSAMA NDO KANIOKOTA JUU YA JALALA
SIWEZI TENA KULALA BORA NIENDE CLUB KUCHEK MIDA SAA TANO ZA USIKU MSALA
NAULI YENYEWE NILIYONAYO YA DALADALA
NAFUNGUA MLANGO NABAMIZA
NINAPITA KICHOCHORO KUNA GIZA GIZA
NAKUTANA NA DU MALAYA
NAMSHANGAA ANALIA
ANADAI AMESHAKOLEA KUJENGA FAMILIA
NAONA DU! BILA DUA NINAMUANGUSHA NGAMIA
MARA NAGUSWA BEGA MCHIZI WAKE KATOKEA DUUUU! BABAKE ANAMAPANA KAJAZIA!

JAMAA unafanya nini na dem wangu?
KIDEM baby alikuwa anataka kunibaka!

DUUU! KUSHOTO KULIA MCHIZI NACHUNGULIA
NAPATA UPENYO NDUKI NADISAPIA
NAPISHANA NA MAAFANDE KAMA SABA WA DORIA
NIKO MKUKU KAMA BENZI SPIDI MIA KWENYE NJIA
BILA KUULIZA KISA MAAFANDE SI WANANIUNGIA
NAHISI KAMA JUMBA BOVU LINANIANGUKIA
WALIO SEMA HII DUNIA NI TAMBARA KA GUNIA
MBONA HALICHANIKI CHINI NIKADUMBUKIA
NAKATA MITA NYINGI MIGUU JUU YA NJIA
BREKI YA KWANZA GETO KWA DEM WANGU FAUDHIA

MIMI ngo ngo ngo faudhia nifungulie fasta
FAUDHIA kwani kuna nini baby?
MIMI aaah zima taa tulale bwana tutaongea kesho
FAUDHIA lakini baby nishakukataza maswala ya kutembea usiku aaaah

KUSINZIA KIDOGO TU WANAKUJA WATU WA HATARI
WANAUPIGA TEKE MOJA TU MLANGO CHALI
WANAZAMA KWANZA JIKONI WANAPAKUA WALI
WANAKULA WANASHIBA KISHA WANAANZA ZALI
WANAMKAMATA DEMU WANGU KISHA WANA MWINGILIA KIMWILI
MBELE YA MACHO YANGU NA ANA MIMBA YA MIEZI MBILI
SINA JINSI NIMEWEKEWA BUNDUKI YA SIKIO
HASIRA ZINAONGOZANA MAPIGO YANAKWENDA MBIO
BAADA YA KUMBAKA DEMU WANGU WANAAMUA KUNITEKA NYARA
WANANIAMBIA SONGESHA NINAONGOZA MSAFARA
KUFIKA NJE WANANIFUNGA KAMBA MIKONO, MIGUU
KISHA WANANIINGIZA NDANI YA COROLA
MWENDO MREFU NINAPITIWA USINGIZI NALALA
NIMEKUJA KUSHTUKA GARI IKO SPIDI BALAAA
KUMESHAPAMBAZUKA ILE MIDA YA SWALASWALA
TUNAFIKA KATIKATI YA ILE MBUGA YA MANYARA
WANAMUONA SIMBA KIDUME ANANJAA HATA NYASI HAJALA
WANANITUPA NINAANZA KUFANYA SALA
MUNGU KWA UWEZO WAKO HUYU SIMBA AGEUKE SWALA
ILE KUFUMBUA MACHO USO KWA USO NA COBRAAAAAA

MWISHO WA PART 1

huu wimbo mimi binafsi nauheshimu sana kutokana na aidia yake mimi nimekuwa msanii wa kwanza duniani kutengeneza wimbo ambao ni movie ya kutisha so kama unaukubali wimbo huu unapatikana katika album ya PASAKA yenye jumla ya nyimbo 23 na inauzwa tsh 5000tu kumbuka wimbo huu huwezi kuupata sehem nyingine yoyote zaidi ya kwenye album ya PASAKA kwa maelezo ya jinsi ya kupata album piga 0756799877 utaongea na mimi mwenyewe na nitakuelekeza wapi utapata album. usibeep wala kutuma sms plz.

SHEA MASHAHIRI HAYA NA MARAFIKI ZAKO ILI NAO WAJIPATIE BURE.
0444

1 comment:

xhobi mzawa said...

mia kaka ngoma imetulia sana itanibidi niitafute hata wana wa RAMBIRAMBI na KIKODIU wamelike hii kitu respect kwako