Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya
Vodacom Mahela,Bw.Valerian Kamugisha, akishuka kwenye ndege mkoani Kigoma nyumbani
kwao na kulakiwa na baba yake mzazi mara baada ya kukabidhiwa pesa zake hapo
juzi
Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya
Vodacom Mahela,Bw.Valerian Kamugisha,akisalimiana na Meneja wa Vodacom Mkoa wa
Kigoma Bw.Kasinde Umella alipowasili uwanja wa ndege Kigoma nyumbani kwao baada
ya kukabidhiwa rasmi pesa zake juzi.
Meneja wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Bw. Kasinde Umella (kulia)akisalimiana
na Baba mzazi wa Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom
Mahela,Mzee Nicodemus Nalisis,alipofika uwanja wa ndege kumlaki kijana wake
Bw.Valerian Kamugisha(katikati)alipowasili Kigoma mara baada ya kukabidhiwa
kitita chake hapo juzi.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya
Vodacom Mahela, Bw.Valerian Kamugisha, akiwaonyesha majirani pamoja na babake
mzazi moja ya picha aliyotolewa kwenye gazeti la Tanzania Daima jinsi
alivyokabidhiwa pesa zake hivi
karibuni,mara baada ya kuwasili mkoani
Kigoma nyumbani kwao.
Mshindi wa
shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Bw.Valerian Kamugisha, akiwaonyesha
majirani pamoja na babake mzazi moja ya picha aliyotolewa kwenye gazeti la Habarileo
jinsi alivyokabidhiwa pesa zake hivi
karibuni,mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma nyumbani kwao.
Baba mzazi wa Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa
Promosheni ya Vodacom Mahela,Mzee Nicodemus Nalisis,akiongea machache mara
baada ya kijana wake Kamugisha kuwasili Kigoma.
Rai hiyo imetolewa na Mzazi wa kijana aliyeshinda shilingi
milioni 100, katika Promosheni ya “VODACOM MAHELA” Bw. Nicodemus Nalisis ametoa
wito kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma kujenga tabia ya kushiriki mashindano mbalimbali
yanayotolewa na kampuni za simu za mkononi hapa nchini
Mzee Nicodemus alisema hayo jana katika uwanja wa ndege
mkoani Kigoma wakati alipowasili kumpokea kijana wake Valerian Nicodemus Kamugisha
aliyewasili mkoani hapa mara baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi milioni 100 juma tatu ya wiki hii
baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Alisema kuwa hatua ya kushiriki mashindano hayo yatatoa
fursa ya ushindi kwa wananchi wengi mkoani Kigoma hivyo kuongeza uwezekano wa
mkoa wa Kigoma kutoa washindi wengi katika mashindano yanayoendeshwa na Vodacom
na kupadilisha maisha yao ya kiuchumi na kimaendeleo kiujumla.
Bw Nicodemasi alieleza kufurahishwa na hatua ya mwanae
kushinda katika shindano hilo nakwamba mbali na hiyo kuwa fedha hizo ni msingi
mzuri wa maisha ya kijana huyo lakini pia ushindi huo ni fahari kwa wananchi wa
Kigoma na historia kubwa ya kijana huyo na familia,alisema ingawaje yeye
alishiriki katika promosheni hiyo bila mafanyikio na mwanae kushinda basi
anampongeza kwani sawa sawa kama yeye kashinda tu.Alisema.
Licha ya kuipongeza Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
kwa mashindano mbalimbali likiwemo la VODACOM MAHELA na kwamba hatua hiyo
inachangia katika kukuza na kupanda uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na familia
kwa ujumla.
Aidha mmoja wa majirani wa familia ya mshindi huyo Bw
Jackson Kakwaya mfanyabiashara wa bidhaa madukani alisema hatua ya ushindi wa
kijana huyo inapaswa kuwa hamasa tosha kwa watu wengi wa mkoa huu kushiriki
katika shindano hilo kikamilifu.
Alisema ushindi huo umemfanya aamini kuwa hakuna upendeleo
katika shindano hilo na hakutarajia kama ingewezakana mkazi wa kigoma kushinda
shindano tena la fedha nyingi kiasi hicho.
Alisisitiza Vodacom kuendeleza program kama hizo hatua
ambayo alisema inawapa fursa washindi kuboresha maisha yao ghafla kutoka katika
hali ya chini au ya kawaida nakuwa tajiri kwa muda mfupi.
Hata hivyo Bw Kakwaya alisisitiza umuhimu wa kijana
aliyeshinda shindano hilo nakunyakuwa milioni 100, kukaa chini na kupanga
mikakati madhubuti itakayo boresha maisha yake na familia badala ya kuzitumia
katika anasa.
Kwa upande wake mshindi wa Vodacom Mahela Bw Valerian Kamugisha
mbali na kupongeza Vodacom kwa kumkabidhi zawadi hiyo alikiri shindano hilo
kutokauwa na mianya yoyote ya rushwa nakusema kuwa hana ndugu katika kampuni
hiyo lakini ameshinda.
Aliwataka wananchi kuamini mashindano yanayoendeshwa na
Vodacom nakushiriki mara kwa mara jambo ambalo litaongeza idadi ya washindi
mkoani Kigoma nakuondoa dhana kuwa Kigoma haiwezi kutoa mshindi ni mwisho wa
reli.
“Hakuna aliyeamini kuwa Kigoma ingeweza kutoa mshindi tena
mtu kama mimi, lakini ndio hivvo
nimeshiriki kikamilifu bila kuchoka hatimaye nimeibuka na milioni 100” alisema
Kamugisha.
Bw Kamugisha pamoja na kushinda alisema ataendelea na
kushiriki mashindano mengine ya Vodacom ili kupata fursa zaidi kushinda fedha
zingine huku akiwashauri wananchi hasa vijana mkoani Kigoma kuchangamkia fursa
hizo kujaribu bahati ili kuboresha maisha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment