22.11.13

Thursday, May 23, 2013

(News) Wakulima sasa kupata taarifa za kilimo kupitia simu

Balozi wa Finland nchini Tanzania, Sinikka Antila akisalimiana na Afisa maendeleo ya Biashara wa Vodacom Tanzania Nixon Bonaventure wakati wa hafla ya kuanzisha Ushirikiano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya Sibenonke ya nchini Finland. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa Mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa Alexander Stubb (katikati). Waziri wa maendeleo ya kimataifa Heidi Hautala ( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni ya Sibenonke Uwe Schwarz. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa balozi huyo. 

Waziri wa mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa wa Finland, Alexander Stubb, akifanya mahojiano na Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Bw.Matina Nkurlu katika hafla ya kuingia katika Ushirikiano utakao wawezesha wakulima kupata taarifa za kilimo kupitia simu za mkononi. Pamoja nao ni Waziri wa maendeleo ya kimataifa Heidi Hautala (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa kampuni ya Sibenonke Uwe Schwarz.
Wakulima sasa kupata taarifa za kilimo kupitia simu
*    Ni kufuatia ushirikiano kati ya Finland na Vodacom
*    Sera ya Kilimo kwanza kuongezewa tija zaidi
Waziri wa Mahusiano ya Ulaya na Biashara za kimataifa wa Finland Alexander Stubb, amesema kuwa nchi yake sasa itawekeza zaidi katika kuwainua wakulima wadogo wa Tanzania kwa kuwawezesha kupata elimu, taarifa na mafunzo mbalimbali ya kilimo na ufugaji kupitia maendelea ya teknolojia.
Hayo yametanabaishwa na Waziri huyo wakati wa hafla ya kuingia katika Ushirikiano kati ya Kampuni ya Sibenonke ya nchini Finland na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom makubaliano yatakayo wawezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo kwa njia ya simu.
Waziri huyo amesema kuwa nchi yake imekuwa ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali na kwa sasa wameona ni vyema kuwekeza zaidi katika kuwasaidia wakulima wadogo ambao pia wamepewa kipaumbele na serikali kupitia sera yake ya Kilimo kwanza.
"Tanzania tangu awali imekuwa kilimo kama uti wa mgongo katika kujenga na kuliendeleza taifa,  tumetambua kuwa jitihada za kuwaendeleza wakulima zimekuwa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa upatikanaji wa taarifa muhimu, Ushirikiano huu sasa utawawezesha wakulima kupata taarifa hizo katika viganja vyao na kwa wakati wowote," alisema Stubb.
Aidha Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa nchi hiyo, Heidi Hautala amesema kuwa ni vyema sasa wakulima wa Tanzania wakabadilika kwa kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija.
"Tanzania kwa kipindi kirefu imekuwa inafanya jitihada kubwa kuwainua wakulima, nasi kwa kushirikiana na kampuni na wadau wengine kutoka nchini Finland tumekuwa tukiwaunga mkono kuhakikisha inawasaidia wakulima kutumia teknolojia za kisasa, Ushirikiano huu utakuwa ni chachu kwa maendeleo ya wakulima wa Tanzania kwani sasa watarahisishiwa kupata taarifa za namna bora ya kuendesha kilimo," Alisema Hautala.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa miundombinu hafifu ya barabara na mawasiliano imekuwa kikwazo kwa wakulima kupata taarifa muhimu za kilimo na mafunzo, Ushirikiano huu wa Vodacom na Sibenonke utakuwa suruhisho kubwa katika kukabiliana na changamoto hizo za kipindi kirefu.
Twissa, aliongeza kuwa Kampuni ya Vodacom imekuwa katika jitihada za kutafuta njia bora katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mtandao wake uliosambaa nchini kote. " Tunafuraha na faraja kuingia katika Ushirikiano na kampuni hii ya Sibenonke," alisema
"Maendeleo ya kilimo yamekuwa na changamoto kubwa kwa taifa hili, mpango huu wa kutoa taarifa kwa wakulima kupitia njia ya simu utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha sekta hii, tunawasihi Watanzania kutumia fursa hii ya kiteknolojia katika kuboresha kilimo nchini na pia kukuza uchumi wa nji yetu", alifafanua Twissa.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Sibenonke,  Uwe Schwarz, amesema ushirikiano huo na kampuni ya Vodacom Tanzania, umekuwa sehemu ya kuendelea kupanuka kwa mtandao wa huduma kwa kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika ya Mashariki ambako maendeleo ya teknolojia yameendelea kuwa changamoto kwa muda mrefu.
"Tunayo furaha kubwa kuingia katika ushirikiano huu na kampuni ya Vodacom katika kuwarahihishia huduma wakulima wa Tanzania, Tunaamini kuwa kwa pamoja tutaleta mapinduzi makubwa katika kilimo kwa kuongeza tija katika uzalishaji na mazao na usalama wa chakula. Suruhisho letu hili lisilo na gharama yoyote italeta maendeleo makubwa kwa Watanzania.
Mwenyekiti wa MOAT bwana Reginald Mengi, amesema kuwa vyombo vya habari vimefanya jitihada kubwa katika kufikisha taarifa kwa wakulima lakini bado changamoto imekuwa kubwa kuwafikia wote kulingana na maeneo waliyopo hivyo kwa Ushirikiano huu anaamini kuwa sasa taarifa zote za msingi zitawafikia wakulima hata walio katika maeneo yasiyofikiwa na vyombo vya habari.
"Ninawapongeza sana Vodacom kwa kuona umuhimu wa kuingia katika ushirikiano huu ambao unaleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini. Sisi kama wadau wa vyombo vya habari tumefanya kazi kubwa hivyo kwa kutumia mtandao wa Vodacom ambao umesambaa nchini kote wakulima sasa wataweza kupata taarifa wanazohitaji kupitia simu zao za Mkononi, Alisema Bwana Mengi.
Mwisho..

No comments: