KUHUSIANA
NA KIFO CHA MSANII ALBERT MANG’WEA.
Kampuni ya QS MHONDA J ENTERTAINMENT tunatoa salumu zetu za rambi rambi
kwa familia ya marehemu ALBERT MANG’WEA ambaye tunatambua na kuthamini mchango wake katika
tasnia ya muziki ambayo inakua kila kukicha hivyo baada ya kutafakari sana kwa
kina uongozi wa kampuni ukaona itakuwa ni jambo jema kama tutaendelea na TAMASHA
la tarehe 01/06/2013 ili
kuwapa mashabiki nafasi ya kuichangia familia ya marehemu katika siku hiyo ya
tamasha ambako kutakuwa na kipindi maalumu siku hiyo ambako kila ambaye atafika
atapa nafasi ya kuichangia familia ya marehemu na tunaamini hii itakuwa ni
nafasi kwa wakazi wa Dar es salaam kutoa rambi rambi zao na kuifikia familia ya
marehem kupitia mwakilishi wa familia ya marehemu na pia sisi kama kampuni
tutatoa mkono wa rambi rambi katika siku hiyo hivyo basi tunaomba wadau wa
burudani wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 01/06/2013 katika ukumbi wa DAR LIVE ili
kuweza kumuombea na pia wasanii mbalimbali wataimba nyimbo za kuomboleza.
No comments:
Post a Comment