WARSHA YA UTENGENEZAJI FILAMU- MAOMBI YAFUNGULIWA
ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji
filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji
filamu wakati wa ZIFF mwaka huu..
Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki)
watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi
5 wengine watajilipia wenyewe.
Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha
watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi
wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu
chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku
ya mwisho.
Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi:
CV fupi.
Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika
la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC)
Maelezo pia yako www.ziff.or.tz
No comments:
Post a Comment